MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Makala > TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa
Makala

TTCL  Yatumia Tamasha La Kizimkazi Kueleza  Wananchi Fursa Wanazotoa

Author
By Author
Share
5 Min Read
Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la KIZIMKAZI 2026  sio jukwaa la utamaduni, burudani na uwekezaji pekee, bali pia limekuwa darasa la wazi lililoonesha namna teknolojia na mawasiliano yanavyoweza
kuwa kichocheo cha biashara, huduma na maendeleo ya Taifa.
Katika tamasha hilo, Shirika la Mawasiliano Tanzania

Habari Picha 13264

(TTCL) lilitumia banda lake la

maonesho kuwa daraja kati ya wananchi na fursa zinazopatikana kupitia teknolojia, huku likitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazolenga kurahisisha maisha, kuongeza ufanisi wa biashara na kuchochea uchumi wa kidijitali.
Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan, na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, walipata fursa ya  kutembelea anda la TTCL pamoja na mabanda mengine 60 yaliyoshiriki katika tamasha  na  kukutana na maofisa na wataalamu waliokuwa
wakihudumia wananchi katika  eneo hilo.
Habari Picha 13265

Habari Picha 13263

Kwa mujibu wa Meneja TTCL,Nasra Mugheir banda la TTCL lilikuwa eneo la kukutana kwa wananchi, wafanyabiashara, taasisi na wataalamu wa TTCL, huku  wageni wakipata nafasi ya kuuliza maswali, kupata maelezo kuhusu huduma za mawasiliano na kufahamu namna teknolojia inaweza kutumika kufungua fursa mbalimbali katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumzia tamasha hilo, Nasra anasema kwa mujibu wa takwimu za TTCL, jumla ya Wananchi 360 wakiwemo Wafanyabiashara, wajasiriamali, Taasisi, Mashirika, Kampuni na wananchi kwa ujumla  walitembelea banda
hilo katika kipindi chote cha maonesho, jambo lililoonesha mwitikio wa wadau katika kutafuta taarifa na huduma za kidijitali.
Hata hivyo, amesema , thamani ya ushiriki huo haikuwa katika idadi pekee, bali katika
mazungumzo yaliyofanyika kati ya wataalamu wa Shirika na wananchi waliotembelea banda hilo.
“Wadau waliofika katika banda la TTCL wakitaka kufahamu namna ya kupata intaneti ya kasi, wengine walitaka kujua huduma za kifedha za kidijitali, huku wafanyabiashara na taasisi wakitafuta suluhisho za TEHAMA zinazoweza kuongeza ufanisi wa shughuli zao,” amesema.
Amesema TTCL  imetumia fursa hiyo  na kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya mtoa huduma na mtumiaji na kwa mwananchi aliyekuwa na swali, alipata mtaalamu wa kutoa ufafanuzi.
Aidha  kwa mfanyabiashara aliyekuwa akitafuta njia rahisi ya kupokea malipo, kulikuwa na maelezo kuhusu huduma za kifedha; na kwa aliyekuwa akihitaji intaneti yenye kasi, kulikuwa na
fursa ya kufahamu huduma zinazopatikana.
Aidha  amesema TTCL imeelezwa kuwa
mawasiliano ya kisasa hayaishii kwenye simu au intaneti kwani kuna  suala la
miundombinu mikubwa inayowezesha taarifa kusafiri kutoka eneo moja hadi nyingine kwa kasi na uhakika.
“Msingi wa miundombinu hiyo ni Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, ambao kwa sasa una zaidi ya kilomita 15,000 za nyuzi za mawasiliano na unaendelea kupanuliwa ili kuongeza uwezo na kufikisha huduma katika maeneo mengi zaidi,” amesema.
Amesema TTCL imepewa jukumu la kusimamia na kuendesha miundombinu hiyo kwa niaba ya Serikali, ikiwa sehemu ya juhudi za kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika huduma za Serikali, elimu, afya, biashara na shughuli nyingine za kiuchumi.
Kuhusu Kituo cha Kuhifadhi  Na Kusimamia Taarifa Kimtandao NIDC, amesema  kina miundombinu ya Tier III na kimeunganishwa na Mkongo wa Taifa, hatua
inayowezesha taasisi na kampuni kupata huduma za data kwa kiwango kinachohitajika  katika mazingira ya kisasa ya biashara.
Amesema uchumi wa kidijitali hauhitaji intaneti pekee. bali mazingira salama na yenye uhakika ya kuhifadhi na usimamizi wa taarifa kitaalam ambapo kupitia huduma za NIDC na Cloud Computing, taasisi zinaweza kutumia miundombinu ya kisasa ya TEHAMA bila kulazimika kuwekeza wenyewe katika miundombinu mikubwa ya kuhifadhi data.
Aidha amewataka wananchi wanaohitaji intaneti ya kasi nyumbani au kazini,
huduma ya Faiba Mlangoni Kwako (FTTH). Huduma hiyo hupeleka intaneti kupitia nyuzi za mawasiliano moja kwa moja hadi kwenye nyumba au eneo la mteja.
Katika tamasha hilo TTCL ilitoa huduma ya
Wi-Fi kuwawezesha washiriki kutumia intaneti , hivyo kufanya teknolojia kuwa sehemu ya uzoefu wao badala ya kubaki
kwenye maelezo ya mabango na vipeperushi.
Kuhusu Dira ya Taifa Ya Maendeleo 2050 amesema,  teknolojia itakuwa sehemu muhimu ya uzalishaji, ushindani, biashara, elimu, huduma za Serikali na ubunifu.
Katika safari hiyo, miundombinu ya mawasiliano ina nafasi ya msingi ambapo kuna Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano unaowezesha maunganisho (connectivity) ya taifa, NIDC inayosaidia taasisi na kampuni kuhifadhi na kusimamia data na mifumo yao na FTTH inayosogeza intaneti ya kasi karibu na nyumba, ofisi na biashara.
Amesema huduma hizo zinaonesha kuwa uchumi wa kidijitali haujengwi na teknolojia moja bali unahitaji mtandao wa mawasiliano, data salama, huduma za fedha kidijitali na intaneti
yenye kasi vyote vikifanya kazi kwa pamoja.

You Might Also Like

OSHA yaelimisha sheria mahala pa kazi kwa JOWUTA

Kenya, Tanzania Zashirikiana na China Kukabiliana na Changamoto za Ushuru wa Marekani

Inzi Chuma: Suluhisho la Chakula cha Mifugo, Uhifadhi wa Mazingira

SmartDarasa: Tunda la Miaka 40 ya COSTECH Linalobadili Elimu ya Sayansi Tanzania

IITA,TARI, TPHPA Wapambana Kudhibiti Ugonjwa Wa Fungashada Ya Migomba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia Afurahishwa Na Huduma za NSSF
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Rais Samia Afurahishwa Na Huduma za NSSF
Habari August 13, 2026
  VETA Yashiriki Tamasha La Kizimkazi
Habari August 13, 2026
Vijana Watakiwa Kuanza Utekelezaji Wa Mipango Waliyonayo
Habari August 12, 2026
TARI Yafanya Majaribio Ya Viazi Mviringo Dodona
Habari August 11, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?