MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TARI Yafanya Majaribio Ya Viazi Mviringo Dodona
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TARI Yafanya Majaribio Ya Viazi Mviringo Dodona
Habari

TARI Yafanya Majaribio Ya Viazi Mviringo Dodona

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
DODOMA: Mkoa wa Dodoma umeanza kuvunja dhana ya kuwa ni eneo linalofaa kwa mazao machache kutokana na ukame, baada ya jaribio la kwanza la viazi mviringo lililofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kuonesha mafanikio makubwa.
Jaribio hilo lililofanyika katika shamba la Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Philip Mpango, Kijiji cha Mayamaya, Wilaya ya Bahi, limedumu siku 104 hadi hatua ya uvunaji na kuthibitisha kuwa zao hilo linaweza kustawi katika mazingira ya Dodoma, likifungua fursa mpya ya chakula, biashara na kuongeza kipato kwa wakulima.
Mafanikio hayo yamekuja wakati wakulima wa Dodoma wakitakiwa kupanua wigo wa mazao badala ya kutegemea mazao machache, huku utafiti na teknolojia za kilimo zikitajwa kuwa njia ya kukabiliana na changamoto za ukame na kuongeza uzalishaji.
Akizungumza baada ya kuvuna viazi hivyo, Dkt. Mpango aliwataka wakazi wa Dodoma kuanza kujiandaa kuchangamkia fursa hiyo mara utafiti utakapokamilika na mbegu hiyo kuanza kutolewa rasmi.
“Wakazi wa Dodoma sasa tuanze kuchangamkia hii fursa na TARI wako tayari kutusaidia kwa kutupatia mbegu bora zinazofaa zaidi. Hii itatusaidia chakula na kipato kwa ajili ya kusaidia watoto wetu kwenda shule,” alisema.
Alisema mafanikio hayo yanaonesha kuwa Dodoma si lazima itegemee mtama, mahindi, zabibu au alizeti pekee, bali inaweza kuongeza mazao mengine kupitia maarifa ya kilimo na matumizi sahihi ya maji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Thomas Bwana, alisema taasisi hiyo inapanga kuendeleza majaribio ya zao hilo kwa wakulima wadogo wanaotegemea mvua, hatua itakayosaidia kutathmini uwezo wa zao hilo katika maeneo mbalimbali.
Alisema TARI itaendelea kufanya tafiti katika maeneo tofauti nchini ili kuondoa dhana kwamba eneo fulani linafaa kwa zao moja pekee, huku akiwataka wakulima kuruhusu taasisi hiyo kufanya majaribio ya teknolojia na mbegu katika mashamba yao.
Mtafiti Kiongozi wa zao hilo kutoka TARI Uyole, Dkt. Owekisha Kwigizila, alisema mbegu hiyo mpya inaweza kukomaa ndani ya takribani siku 90, kustahimili ukame na baadhi ya magonjwa, huku ikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 35 hadi 40 kwa hekta moja.
Wakazi wa Mayamaya walioshiriki katika uvunaji huo walisema wamevutiwa na namna zao hilo lilivyostawi katika eneo hilo na kuonesha utayari wa kuanza kulima endapo utafiti utakamilika na mbegu kupatikana.

You Might Also Like

Muhogo, viazi kuongezewa tija kwenye uzalishaji

Rais Dk Mwinyi Kukata Keki Sabasaba

Majaliwa Asema Sekta ya Uvuvi Yaingiza trilioni 2.9 kwa Mwaka 

Uongozi OUT Waahidi Kuboresha Mazingira ya Kazi

Ridhiwan Azindua Jengo La Biashara La TUCTA-Arusha

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Shilingi Milioni 28 Zilivyogeuza Wazo Kuwa Mashine Ya Shambani
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Shilingi Milioni 28 Zilivyogeuza Wazo Kuwa Mashine Ya Shambani
Makala August 11, 2026
Bima Ya Afya Kwa Wote: Safari Ya Kumfikia Kila Mwananchi
Makala August 11, 2026
Mabilika Kutoka Ubunifu Hadi Soko La Afrika
Makala August 9, 2026
TARURA Yafungua Njia Mpya Kukwepa Msongamano Dodoma
Habari August 9, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?