MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima
Habari

TPHPA Kuja Na Ramani Ya Visumbufu Nchi Nzima

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Lucy Ngowi

DODOMA: MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) imeanza mpango wa kupanua uchunguzi wa visumbufu vya mazao katika maeneo mbalimbali nchini, kwa lengo la kutengeneza ramani ya kitaifa itakayoonyesha mtawanyiko wa visumbufu na kuwawezesha wakulima kutumia viuatilifu sahihi kwa wakati na katika maeneo husika.

Hatua hiyo inalenga kubadili mfumo wa udhibiti wa visumbufu kutoka matumizi ya viuatilifu kwa mazoea kwenda kwenye udhibiti unaotegemea taarifa sahihi za kisayansi, hatua inayotarajiwa kupunguza gharama za uzalishaji, hasara za mazao na matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu.

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane, Profesa Joseph Ndunguru kutoka TPHPA, amesema mamlaka imeanza kupata taarifa muhimu kupitia teknolojia inayowezesha kubaini visumbufu vya mazao, ikiwemo bakteria, virusi, fangasi na wadudu, hata pale ambako dalili zake haziwezi kuonekana kwa macho.

Amesema ramani hiyo itakapokamilika, itawezesha wataalamu na wakulima kufahamu aina za visumbufu vinavyopatikana katika maeneo mbalimbali na kupanga hatua za udhibiti kulingana na tatizo lililopo.

“Ukipeleka kiuatilifu sahihi katika eneo sahihi na kudhibiti kisumbufu sahihi, tunapata udhibiti endelevu wa visumbufu,” amesema.

Amesema uchunguzi uliofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa umeonyesha umuhimu wa teknolojia hiyo, baada ya kubaini visumbufu mbalimbali katika mazao ya mihogo, vitunguu, karanga, Chinese cabbage na sukuma wiki.

Kwa mujibu wa Profesa Ndunguru, katika mihogo zilibainika changamoto zinazohusisha utitiri, bakteria na fangasi, wakati vitunguu vilibainika kuwa na visumbufu vinane, vikiwemo bakteria na fangasi.

Amesema katika karanga vilibainika visumbufu vitatu, ikiwemo kirusi kinachoweza kusababisha majani kuwa ya njano na mimea kudumaa, huku Chinese cabbage ikiwa na visumbufu sita na sukuma wiki ikibainika kuwa na bakteria, fangasi na virusi.

Amesema taarifa hizo zitasaidia TPHPA na wataalamu wa kilimo kutoa mapendekezo sahihi ya udhibiti kwa kuzingatia aina ya kisumbufu na eneo kinapopatikana, badala ya wakulima kutumia dawa kwa kubahatisha.

Naye Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Mpwapwa, Salum Ally, amesema teknolojia hiyo imewasaidia wataalamu kubaini changamoto ambazo haziwezi kuonekana kwa macho na kutoa ushauri unaoendana na tatizo halisi la mazao.

Ameomba uchunguzi huo kupanuliwa katika maeneo mengi zaidi nchini ili wakulima wanufaike na taarifa sahihi kuhusu visumbufu na namna bora ya kuvidhibiti.

You Might Also Like

Wachimbaji Wadogo Wafikiwa

Wasilisheni Migogoro Yenu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi – Massawe

Wakulima wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea

USAID yatoa Dola mil nane Kwa kampuni za Tanzania

Rais Samia atoa zaidi ya bil. 2.1 usimikaji wa mifumo, uendeshaji mashauri ya wafanyakazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Dkt. Samia: Ushirika Simamieni Matrekta Kwa Manufaa Ya Wakulima
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Dkt. Samia: Ushirika Simamieni Matrekta Kwa Manufaa Ya Wakulima
Habari August 9, 2026
Jeshi La Zimamoto Yaimarisha Elimu Kwa Wananchi Kuhusu Matumizi Salama Ya Nishati Ya Kupikia
Habari August 9, 2026
DC Kondoa  Aipongeza TFS Kwa Teknolojia Ya Uhifadhi Wa Misitu Na Utali
Habari August 8, 2026
Waziri Nanauka Aipongeza   TARURA Kwa Mpango Wa  CBRM ‎
Habari August 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?