MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT
Habari

Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti na Uchumi Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Suleiman Misango (kulia), akizungumza mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko wa PSSSF,, Hajj Moshi.
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: MKURUGENZI wa Tafiti na Uchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Suleiman Misango, amepongeza mfumo wa kidijitali wa PSSSF Portal baada ya kushuhudia jinsi unavyowezesha taarifa za wanachama kupatikana kwa haraka, akisema ni hatua kubwa ya kuboresha utoaji wa huduma za hifadhi ya jamii.
Dkt. Misango ametoa pongezi hizo, baada ya kuhudumiwa katika banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwenye Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma.
Amesema alishangazwa na kasi ya mfumo huo baada ya kutaja jina lake na kuona taarifa zake zote za uanachama, kuanzia alipoanza ajira hadi sasa, zikionekana mara moja.
“Mimi ni mwanachama wa PSSSF wa muda mrefu, lakini nilipotaja tu jina langu, taarifa zangu zote zikaonekana mara moja. Hii inaonesha mfumo umeboresha sana utoaji wa huduma,” amesema.
Habari Picha 13127

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Tafiti na Uchumi Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Suleiman Misango (katikati), akizungumza mbele ya Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa PSSSF, Hajj Moshi (kushoto) na Meneja Mawasiliano wa BoT,  Vicky Msina, kwenye Maonesho ya Nanenane Viwanja vya Dkt. John Malecela jijini Dodoma Agosti nne, 2026

Ameongeza kuwa tofauti na ilivyokuwa zamani, ambapo watumishi walilazimika kutafuta mafaili kwa muda mrefu, sasa taarifa zinapatikana kwa kubonyeza kitufe kimoja, hatua inayorahisisha upatikanaji wa huduma popote kupitia PSSSF Portal.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSSSF,  Hajj Moshi, amesema Mfuko unaendelea kuhamasisha wanachama kutumia PSSSF Portal ili wajihudumie kwa urahisi popote na wakati wowote.
Amesema matumizi ya mfumo huo yameongeza ufanisi wa huduma na kusaidia utekelezaji wa kampeni ya “Tunalipa Jana”, inayowezeshwa na utunzaji bora wa kumbukumbu, matumizi ya teknolojia ya kidijitali na uwezo wa kifedha wa Mfuko.
Aidha, amesema maonesho hayo yanatoa fursa ya kuwafikia wanachama, kuwapatia elimu kuhusu huduma za kidijitali na kuwaunganisha na mfumo wa PSSSF Portal, ambao umeendelea kukidhi mahitaji ya wanachama, hususan vijana wanaopendelea huduma za kidijitali.
Katika ziara hiyo, Moshi ametembelea mabanda mbalimbali, yakiwemo ya Taasisi za Elimu ya Juu, Ofisi ya Rais na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), ambapo alizungumza na wanachama na kupokea maoni yao kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko.

You Might Also Like

Kusiluka aitaka TVLA kuongeza tafiti za chanjo 

Kituo Cha Umahiri Cha Upandikizaji Figo, Mafunzo, Kujengwa Hospitali Ya Benjamin Mkapa

Dira za Maji Kumaliza Kero ya Ankara

VETA Yafanya Mageuzi Makubwa Yaliyowezesha Wengi Kuajiriwa

Mpogolo Aipongeza Halmashauri Maandalizi Mikopo Asilimia 10

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam
Habari August 5, 2026
Balozi Wa Kudumu Wa Mashirika Ya UN Atembelea FAO Nanenane
Habari August 5, 2026
Wadau Wamiminika Banda La REA Katika Maonesho Ya Nanenane  2026
Habari August 5, 2026
FAO Yatoa Mafunzo Kwa Wadau Wa Uvuvi Kutumia Teknolojia Zinazoboresha Uzalishaji Mazao Ya Uvuvi
Habari August 5, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?