MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: FAO Yatoa Mafunzo Kwa Wadau Wa Uvuvi Kutumia Teknolojia Zinazoboresha Uzalishaji Mazao Ya Uvuvi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > FAO Yatoa Mafunzo Kwa Wadau Wa Uvuvi Kutumia Teknolojia Zinazoboresha Uzalishaji Mazao Ya Uvuvi
Habari

FAO Yatoa Mafunzo Kwa Wadau Wa Uvuvi Kutumia Teknolojia Zinazoboresha Uzalishaji Mazao Ya Uvuvi

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Lucy Lyatuu, Dodoma
MRADI  wa FISH4ACP  unaotekelezwa na Shirika La Kilimo La Umoja Wa Mataifa (FAO) umewezesha wadau katika mnyororo wa thamani wa uvuvi, wakiwemo wavuvi, wachakataji, wasafirishaji na wauzaji wa mazao ya uvuvi, kutumia teknolojia  bora za kuboresha uzalishaji wa mazao ya uvuvi.
Aidha matumizi ya teknolojia hizo yamewezesha kupunguza kwa kiasi kikubwa  cha upotevu wa mazao ya uvuvi nchini, kupitia mafunzo ya uchakataji, matumizi ya teknolojia za kukaushia na kubanikia samaki pamoja na mifumo ya baridi inayotumia nishati ya jua na umeme.
Kadhalima , FAO kupitia FISH4ACP imeanzisha mfumo wa kidijitali wa TANFISH MARKET unaowaunganisha wauzaji na wanunuzi wa mazao ya uvuvi kutoka maeneo mbalimbali, huku mfumo huo ukiwa na utaratibu wa malipo unaolinda fedha za pande zote mbili kwa kuhakikisha muuzaji analipwa baada ya mnunuzi kupokea mzigo.
Mtaalam wa Mnyororo wa thamani wa Uvuvi na Ufugaji wa Samaki kutoka FAO Hashimu Muumin amesema  FISH4ACP ni mradi wa miaka sita unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Ujerumani na kutekelezwa na FAO, ulioanza mwaka 2020 na unatarajiwa kukamilika Desemba 31, 2026.
 Amesema mradi huo unalenga kuwawezesha wadau katika mnyororo wa thamani wa uvuvi, wakiwemo wavuvi, wachakataji, wasafirishaji na wauzaji wa mazao ya uvuvi, huku ukijumuisha pia shughuli za ufugaji wa viumbe maji na kilimo cha mwani.
Amesema wakati mradi huo unaanza, upotevu wa mazao ya uvuvi ulikuwa ukifikia asilimia 40 na katika msimu wa mvua uliongezeka hadi asilimia 70, hali iliyochangiwa na umbali wa maeneo ya uvuvi kutoka kwenye masoko, upungufu wa miundombinu ya kuhifadhia na kusafirisha mazao pamoja na changamoto katika mifumo ya uchakataji.
Kutokana na hali hiyo, FAO ilitoa mafunzo kwa wadau kuhusu uchakataji, ubanikaji na ukaushaji wa dagaa, sambamba na kuweka mifumo ya barafu na majokofu yanayotumia nishati ya jua na umeme.
Kwa mujibu wa Muumin hatua hizo zimepunguza kwa kiwango kikubwa uharibifu wa samaki na mazao mengine ya uvuvi, huku utafiti uliofanywa katika masoko ya ndani ukibaini kuwa asilimia 96 ya walaji wa samaki kutoka mnyororo wa Ziwa Tanganyika wanapendelea bidhaa zilizohifadhiwa katika hali ya baridi (frozen).
Kutokana na mahitaji hayo, mradi umewezesha kuwekwa kwa mitambo ya kutengeneza barafu na kuwapatia baadhi ya wachakataji majokofu yanayotumia nishati ya jua, hususan katika maeneo yasiyokuwa na umeme.
Kuhusu  mfumo wa kidijitali wa TANFISH MARKET amesema  unawaunganisha wauzaji na wanunuzi wa mazao ya uvuvi kutoka maeneo mbalimbali, huku mfumo huo ukiwa na utaratibu wa malipo unaolinda fedha za pande zote mbili kwa kuhakikisha muuzaji analipwa baada ya mnunuzi kupokea mzigo.
Muumin amesema mradi ulianza katika Ziwa Tanganyika na baada ya kuwafikia wadau wa Ziwa Victoria na maeneo ya Bahari ya Hindi, wameonyesha nia ya kuutumia ili kuongeza fursa za masoko.
Mradi pia umewezesha ujenzi wa Solar Tents katika vijiji zaidi ya 25 vya Ziwa Tanganyika kwa ajili ya ukaushaji bora wa dagaa, ambapo takribani asilimia 95 ya wachakataji wanaonufaika ni wanawake.
Habari Picha 13099
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo, Amina Adrian Kasige, ambaye ni mvuvi na mchakataji na mmiliki wa vyombo vyabuvuvi, amesema teknolojia na elimu aliyoipata kupitia FAO imeongeza kipato chake baada ya kuacha mbinu za zamani za kukaushia dagaa kwenye mchanga, zilizokuwa zikisababisha bidhaa kukosa soko.
 Amesema sasa wanauza dagaa katika masoko ya ndani na nje ya nchi, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda.
 Kwa kuwa FISH4ACP unakaribia kukamilika, ametoa wito kwa Serikali, taasisi, wafadhili na wadau wa maendeleo kuendeleza programu hiyo, akisema teknolojia zilizowekwa tayari zinatumika, zimeonyesha manufaa na bado kuna mahitaji makubwa ya kuendelea kuimarisha mnyororo wa thamani wa uvuvi.

You Might Also Like

Katambi Ahimiza Udhibiti wa Bidhaa Duni, Jamii Yatakiwa Kutumia Huduma za TBS

Elimu ya Ufundi Yachangia Maendeleo ya Taifa – VETA

Majaliwa Aipongeza TPHPA kwa Kuhakikisha Usalama wa Chakula Nchini

Bashungwa Asema Wafungwa Kupewa Mafunzo Ya Ufundi Stadi

Nchi Za SADC Zahimizwa Kutunza, Kulinda Amani

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article IITA, TARI Wabuni Teknolojia Inayoharakisha Uzalishaji Wa Mbegu  Bora Za Muhogo
Next Article Wadau Wamiminika Banda La REA Katika Maonesho Ya Nanenane  2026
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mfumo Wa Kidijitali Wa PSSSF Wamvutia Mkurugenzi Wa BOT
Habari August 5, 2026
FAO Yasisitiza Kutowapa Mifugo Dawa Bila Maelekezo Ya Watalaam
Habari August 5, 2026
Balozi Wa Kudumu Wa Mashirika Ya UN Atembelea FAO Nanenane
Habari August 5, 2026
Wadau Wamiminika Banda La REA Katika Maonesho Ya Nanenane  2026
Habari August 5, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?