NAIBU Waziri Wa Ofisi ya Rais, Tawala Za Mikoa Na Serikali Za Mitaa,(TAMISEMI), anayeshughulikia masuala ya afya Dkt Jafar Rajab Seif amewataka wananchi wenye changamoto mbalimbali ikiwemo uhamisho wa wanafunzi kutumia banda la Waziri Mkuu kupata suluhu.
Amesema hayo alipotembelea banda hilo na kwamba changamoto hizo zinaweza kutatuliwa kupitia banda hilo ambalo linakutanisha taasisi zote zilizopo chini ya Waziri Mkuu,lililoko katika maonesho ya 50 ya biashara ya kimataifa maarufu kama sabasaba.
Amesema banda la Waziri Mkuu katika maonesho hayo limekutanisha kwa pamoja taasisi zilizoko chini yake zikitoa huduma kwa wakati na kwa ufasaha na weledi kwa kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitatua.
“Kwa hizi siku zilizosalia wananchi waje hasa wenye changamoto ya uhamisho wa wanafunzi wao waliopangwa eneo ambalo kuna changamoto za kufika huko,” amesema na kuongeza kuwa watahudumiwa kwa wakati.
Amesema katika banda hilo kuna huduma mbalimbali za uwekezaji,masuala ya afya,huduma za ujenzi wa barabara mijini na vijijini,nahata wanaofuatilia mafao kaa wafanyakazi na wenye changamoto kazini pia wanaweza kupata huduma.
Aidha amesema katika banda hilo wananchi wanaweza kupata huduma ya elimu yammasuala mbalimbalinhivuo wananchi watumie fursa hiyo kwa ajili ya kupata manufaa.