MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watumishi 7881 Watakaostaafu 2026/27 Watambuliwa Kupitia Kampeni Ya Tunalipa Jana-PSSF
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Uncategorized > Watumishi 7881 Watakaostaafu 2026/27 Watambuliwa Kupitia Kampeni Ya Tunalipa Jana-PSSF
Uncategorized

Watumishi 7881 Watakaostaafu 2026/27 Watambuliwa Kupitia Kampeni Ya Tunalipa Jana-PSSF

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu

MKURUGENZI wa Uendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishji wa Umma (PSSSF), Hajj Khamisi amesema Wanachama 7,881 wanaotarajiwa kustaafu utumishi wa Umma katika mwaka huu wa fedha 2026/27 tayari wameambuliwa.

Hatua hiyo inatokana na utekelezaji wa ufanisi wa kaulimbiu ya ‘Tunalipa Jana’.

Khamisi amesema hayo katika Banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere.

“ Tulikwisha wasiliana na waajiri tangu Machi, 2026 kwa kuwapatia orodha ya majina na tarehe za kustaafu kwa watumishi hao,“ amesema huku akiwashukuru waajiri kwa kuonyesha ushirikiano kwa kuwasilisha madai ya watumishi kwa wakati hatua inayourahisishaia Mfuko kuyachakata madai hayo kwa wakati.

Habari Picha 12733

“ Hii itasaidia azma ya Mfuko kutekeleza kaulimbiu yake ya ‘Tunalipa jana’ na hivyo kuwaletea tabasamu wastaafu wetu,” amesema.

Kuhusu mkakati wa kuhakikisha Mfuko unatekeleza kaulimbiu hiyo Mkurugenzi wa TEHAMA, Eric Kato, amesema mifumo ya TEHAMA ya Mfuko imeimarishwa kwa kiasi kikubwa hali inayosaidia uharakishwaji wa utoaji huduma.

“ Kupitia Mifumo, mwanachama anaweza kuwasilisha madai yake mahali popote alipo, hawahitaji kusafiri na hivyo wanaokoa fedha lakini pia Serikali kupitia Mfuko imeokoa fedha nyingi hususan za manunuzi ya karatasi, kwani karibu asilimia 100 ya huduma zinatolewa kupitia mtandao.” Amesisitiza.

Habari Picha 12734

Aidha Mkurugenzi wa Fedha, PSSSF, Ali Yakiti, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeuwezesha Mfuko kwa kuwasilisha michango bila kuchelewesha.

“ Hakuna sababu yoyote kwa Mwanachama pindi anapostaafu acheleweshewe Mafao yake yawe ya Mkupuo au Pensheni ya kila mwezi, tuna slogan ya tunalipa jana tukimaanisha kwamba mwanachama hacheleweshwi kupata haki zake pindi anapotimiza wajibu wake,” amefafanua.

Kwa upande wao, wastaafu wanaopokea pensheni kupitia Mfuko huo, wamesema pensheni zao za kila mwezi wamekuwa wakipata kwa wakati.

“ Pensheni yangu napata vizuri, tarehe 22 wakati mwingine tarehe 23 au 24 haijawahi kuchelewa, nashukuru sana,” amesema Margareth Onjari.

“ Tena wakati mwingine pensheni inawahi mfano mwezi uliopita imewahi vizuri sana, nafikiri labda ni kwa sababu ya maendeleo ya kiteknolojia, sijaona tatizo lolote PSSSF.” Alisema Mstaafu mwingine Said Mohammed.

You Might Also Like

Bil.19 kusambaza umeme vitongojini Tabora

June 20, 2026

Waziri Aweso Aainisha Mikakati ya Kuboresha Huduma ya Maji

Wasira akipongeza Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  kwa kuenzi Falsafa za Baba wa Taifa

Trilioni 1.2 kuboresha miundombinu Mkoa wa Dar es Salaam

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Katambi Apongeza Zimamoto Kwa Uwekezaji Wa Vifaa Vya Kisasa
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Katambi Apongeza Zimamoto Kwa Uwekezaji Wa Vifaa Vya Kisasa
Uncategorized July 7, 2026
Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Habari June 29, 2026
WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Habari June 28, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?