MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: ‎NIRC Imechimba Visima 362, , Yahamasiha Wakulima Kunufaika Na Program Ya Umwagiliaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > ‎NIRC Imechimba Visima 362, , Yahamasiha Wakulima Kunufaika Na Program Ya Umwagiliaji
Habari

‎NIRC Imechimba Visima 362, , Yahamasiha Wakulima Kunufaika Na Program Ya Umwagiliaji

Author
By Author
Share
3 Min Read

‎‎Na Lucy Lyatuu, Dodoma
‎TUME ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) imesema katika kutekeleza programu ya uchimbaji wa visima kwa ajili ya shughuli za umwagiliaji, hadi sasa imechimba visima 362 katika mikoa minne juhudi hizo zikilenga kuongeza uhakika wa uzalishaji wa mazao kwa wakulima wadogo nchini.

Imetaja mikoa ambayo hadi sasa imefikiwa kwa uchimbaji huo kuwa ni pamoja na Geita, Tabora, Manyara na Singida.
‎
Mkurugenzi Msaidizi wa Eneo la Utafiti anayesimamia programu ya uchimbaji wa visima, Naomi Mcharo, amesema hayo wakati ‎akizungumza na katika banda la tume hiyo kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma,.

Amesema Serikali imeanzisha huduma hiyo kufuatia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan yaliyolenga kuwasaidia wakulima kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia kilimo cha umwagiliaji chenye uhakika.
‎
‎Amesema visima hivyo vimekuwa vikilenga zaidi kuwafikia wakulima wadogo, ambapo kisima kimoja kimekuwa na uwezo wa kuhudumia takribani hekari 40 zinazolimwa na wakulima wasiopungua 16 wenye mashamba ya kati ya hekari mbili hadi mbili na nusu kila mmoja.
‎
‎“Mpaka sasa tumeshachimba visima 362 na mashine zetu ambazo Serikali ilitusaidia kuzinunua zinaendelea na kazi katika mikoa ya Mara, Njombe na Mtwara. Lengo letu ni kuhakikisha programu hii inawafikia wakulima wengi zaidi nchini,” amesema Mcharo.
‎
‎Ameongeza kuwa tume imekuwa ikishirikiana na halmashauri za wilaya kutambua na kuhakiki vikundi vya wakulima vinavyonufaika na programu hiyo, huku kila wilaya ikianza na visima vitano katika hatua ya kwanza. Aidha, amesema wakulima binafsi wenye mashamba ya kuanzia hekari 20 hadi 40 wanaweza kuwasilisha maombi kwa tume ili kuchimbiwa visima kwa utaratibu maalumu unaojumuisha ruzuku ya asilimia 20 ya gharama za uchimbaji.

Habari Picha 12586

‎
‎Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2026 yameanza Juni 16 katika Viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23, huku taasisi mbalimbali za umma zikiendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kuhusu huduma wanazozitoa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Maria Itembe, amesema wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kupata taarifa kuhusu huduma za umwagiliaji zinazotolewa na taasisi hiyo.
‎
‎Amesema tume hiyo imeendelea kusimamia ujenzi wa miundombinu mipya ya umwagiliaji, ukarabati wa miundombinu ya zamani, ujenzi wa mabwawa pamoja na uchimbaji wa visima katika maeneo yenye ukame ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
‎

‎
‎
‎

You Might Also Like

Hospitali ya Temeke kufanyiwa maboresho eneo la huduma Kwa wateja

Mradi wa Maadili Katika Utafiti Wa Binadamu Na Huduma Za Afya Wafanywa UDSM kwa Ushirikiano wa Kimataifa

Sababu Nne Zilizofanikisha Mafanikio Katika Uandikishaji

Vijana Wahimizwa Kuweka Akiba

Katibu Mkuu CCM Dkt. Nchimbi Akutana na Katibu Mkuu CRC

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Katibu Mkuu Uchukuzi Aipongeza TASAC,  Kuelimisha Wananchi 
Next Article TAA Yasisitiza Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TMA Yatoa Elimu ya Hali ya Hewa kwa Wananchi Dodoma
Habari June 23, 2026
TAA Yasisitiza Uwajibikaji katika Utoaji wa Huduma
Habari June 23, 2026
Katibu Mkuu Uchukuzi Aipongeza TASAC,  Kuelimisha Wananchi 
Habari June 22, 2026
Qwaray Aipongeza VETA kwa Kukuza Ujuzi wa Vijana
Habari June 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?