MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Yawahamasisha Vijana Kurasimisha Ujuzi Kupitia Programu ya Mama Samia
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Yawahamasisha Vijana Kurasimisha Ujuzi Kupitia Programu ya Mama Samia
Habari

Serikali Yawahamasisha Vijana Kurasimisha Ujuzi Kupitia Programu ya Mama Samia

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu

DAR ES SALAAM: SERIKALI imewahimiza vijana nchini kuchangamkia Programu ya Mama Samia ya Utambuzi na Urasimishaji wa Ujuzi inayotekelezwa hadi Juni 2027, ikilenga kutambua, kuthibitisha na kurasimisha ujuzi walioupata kupitia uzoefu wa kazi, mafunzo kazini na njia nyingine zisizo rasmi za kujifunza.
Akizungumza katika Mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Furahika kilichopo Buguruni Malapa, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,  Wanu Hafidh Ameir, amesema Serikali itaendelea kuimarisha elimu ya ujuzi na umahiri ili kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kushindana katika soko la ajira.
Habari Picha 12517
Amesema programu hiyo inalenga kuwafikia vijana 80,000 nchini na kuwapa fursa ya kutambulika rasmi kwa ujuzi walionao, hata kama hawakupitia mfumo rasmi wa elimu.
“Kupitia programu hii hakuna ujuzi unaopotea kwa kukosa utambuzi rasmi. Niwasihi vijana wote wenye ujuzi walioupata nje ya mfumo rasmi kujitokeza na kutumia fursa hii kurasimisha ujuzi wao,” amesema Wanu.
Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuunganisha mafunzo yanayotolewa vyuoni na mahitaji halisi ya soko la ajira kwa kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za elimu, sekta binafsi na viwanda, hatua inayolenga kuongeza umahiri unaohitajika katika mazingira ya kazi.
Wanu pia amepongeza Chuo cha VETA Furahika kwa mchango wake katika kuwawezesha vijana kupata stadi za kazi, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Bakari Shingo, kwa kusaidia vijana wengi kupata mafunzo ya ufundi.
“Nimeelezwa kuwa Mhe. Shingo amefadhili wanafunzi 220, baadhi yao wakihitimu leo. Haya ni mafanikio makubwa yanayotokana na ushirikiano mzuri kati ya Serikali na wadau wa maendeleo,” amesema.
Aidha, amewataka wahitimu kutumia elimu na ujuzi walioupata kujenga ajira na fursa za maendeleo, huku akisisitiza umuhimu wa nidhamu, ubunifu, uzalendo na ujasiriamali katika kufanikisha ndoto zao na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
Kwa upande wake, Mbunge wa Ukonga, Bakari Shingo, amesema amefadhili wanafunzi 220 katika chuo hicho kwa kutumia utaratibu wa kutangaza fursa kupitia gari la matangazo ili kuwafikia vijana wengi zaidi wanaohitaji mafunzo ya ufundi.
Naye Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. David Cleopa Msuya, amesema chuo kina wanafunzi 460 na kinatoa kozi mbalimbali za ufundi zikiwemo Usimamizi wa Hoteli, Kompyuta, Umeme, Urembo, Ushonaji, Utalii pamoja na Uondoshaji Mizigo Bandarini.

You Might Also Like

Huduma ya Mahakama ya Mwanzo yasogezwa Wilaya ya Ubungo

DART Toeni Fursa Kwa Watanzania Kuwekeza kwenye Mwendokasi -Mchengerwa

TEN/MET, LHRC Zataka Iwekwe Marufuku Matumizi Ya Viboko

Ulega : Nimeridhisha Na Hatua Iliyofikiwa, Ongezeni Kasi Zaidi

Profesa Anangisye Atoa Neno Kwa Wahitimu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Msigwa Asisitiza Mabonanza Ya Michezo Na Sio Kukusanyika Kuvuruga Amani
Next Article ILO Yazindua Mwongozo Wa Habari Za Uhamiaji, Jowuta Yatia Neno
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

OUT Yazindua Programu Mpya za Masomo Kukidhi Mahitaji ya Uchumi wa Kisasa
Habari June 21, 2026
BRELA Yahimiza Urasimishaji Biashara  Kuongeza Fursa Za Ukuaji
Habari June 21, 2026
ILO Yazindua Mwongozo Wa Habari Za Uhamiaji, Jowuta Yatia Neno
Habari June 20, 2026
Msigwa Asisitiza Mabonanza Ya Michezo Na Sio Kukusanyika Kuvuruga Amani
Habari June 20, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?