MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: SELF Yahamasisha Wananchi Kunufaika na Mikopo Nafuu ya Maendeleo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > SELF Yahamasisha Wananchi Kunufaika na Mikopo Nafuu ya Maendeleo
Habari

SELF Yahamasisha Wananchi Kunufaika na Mikopo Nafuu ya Maendeleo

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA:MFUKO wa Self Microfinance Fund (SELF) umeendelea kuhamasisha wananchi kutumia fursa za mikopo nafuu zinazotolewa na taasisi hiyo ili kukuza biashara, kuongeza uzalishaji na kuboresha hali ya maisha kupitia uwekezaji katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma, Meneja wa SELF Kanda ya Kati, Aristid Tesha, amesema mfuko huo umejikita katika kuwafikia wananchi wa makundi mbalimbali kwa huduma za kifedha zinazolenga kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Amesema SELF ina mtandao wa matawi 12 nchini unaohudumia Tanzania Bara na Zanzibar, huku Kanda ya Kati ikihudumia mikoa ya Dodoma na Singida.
“Tumejitokeza kwenye maonesho haya kutoa elimu kuhusu huduma za mikopo, ujasiriamali na usimamizi wa fedha. Wananchi wengi wamekuwa wakitembelea banda letu kupata taarifa na kufahamu namna wanavyoweza kunufaika na huduma tunazotoa,” amesema Tesha.
Kwa mujibu wa Tesha, SELF inatoa mikopo kwa watu binafsi wanaojishughulisha na shughuli halali za kiuchumi, pamoja na mikopo maalumu ya nishati safi inayowawezesha wafanyabiashara wa gesi, vifaa vya umeme na teknolojia za nishati ya jua kupata mitaji kwa masharti nafuu.
Aidha, mfuko huo hutoa mikopo ya jumla kwa vyama vya ushirika na taasisi ndogo za fedha zinazowakopesha wakulima, wafugaji na wananchi wa maeneo ya vijijini, hatua inayolenga kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na walengwa.
Ameongeza kuwa watumishi wa umma wanaweza kupata mikopo kupitia mfumo maalumu uliowekwa na mfuko huo, huku wananchi wengine wakinufaika na mikopo ya kuboresha makazi kwa ajili ya ukarabati au ukamilishaji wa nyumba zao.
Tesha amesema pia vikundi vya kijamii, SACCOS, wakulima na wafugaji wanaoshiriki katika minyororo ya thamani ya mazao na mifugo wana nafasi ya kupata mikopo inayowawezesha kuongeza uzalishaji na kuimarisha shughuli zao.
Mbali na huduma za mikopo, SELF pia hutoa huduma za bima za nyumba, vyombo vya moto na mali nyingine, sambamba na kutoa elimu ya bima kwa wananchi.
Ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda la SELF kabla ya kuhitimishwa kwa maadhimisho hayo ili kupata elimu zaidi na kujionea fursa mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

You Might Also Like

Makamu wa Rais Azindua Mpango wa Kukuza Ujuzi, Ajira kwa Vijana

Washauri Somo la Astronomia Kurudishwa Mashuleni, Kukuza Utalii Anga

Profesa Ndunguru: Tumewezesha Usafirishaji wa Mazao Mbalimbali Yenye Thamani ya Trilioni 15.6

Nishati Safi Ya Samia Yawafikia Wanawake chalinze

Chinyeli Aahidi Chakula Bure kwa Wazee, Mwanyemba Kupambana Kutafuta Maendeleo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article BRELA Kuleta Mradi Wenye Suluhu Kwa Wakulima Na Wafugaji
Next Article BRELA Yahamasisha Urasimishaji wa Biashara kwa Ukuaji wa Uchumi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Hananja Awataka Vijana Kufikiri Mara Mbili Kabla ya Kufuata Wito wa Maandamano
Habari June 18, 2026
June 18, 2026
Habari June 18, 2026
Magereza Yaomba Jamii Kuwapokea Wafungwa Wanaorejea Kutumikia Taifa
Habari June 18, 2026
TPHPA Yasisitiza Matumizi Sahihi ya Viuatilifu kwa Wakulima
Habari June 18, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?