Na Lucy Lyatuu, Dodoma
SERIKALI imetoa taarifa ya hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2025 na kubainisha kuwa imeendelea kutoa huduma za tiba bure na utengemano kwa watu wenye uraibu wa dawa za kulenya ambapo jumla ya watu 85,425 walipata tiba .
Aidha imesema mapambano dhidi ya dawa za kulevya yameendelea kuimarika nchini na kwa mwaka 2025 serikali imefanikiwa kupunguza upatikanaji wa dawa za kulevya,kupunguza uhitaji,kupunguza madhara na kuimarisha ushirikiano wa kitaifa,kikanda na kimataifa.
Kadhalika imesema katika kipindi cha mwaka 2025 kuliibuka aina mpya ya dawa za kulevya ainamya kratom itokanayo na mmea unaoitwa mitrogyna specious ambapo tani 29.52 zilikamatwa jijini Dar es Salaam,dawa hiyo iliingizwa nchini kama mbolea,baada ya uchunguzimikabainika kuwa ni dawa ya kulevya.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Uratibu na wenye Ulemavu), Profesa Palamaganba Kabudi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kumbi za Bunge jijini hapa ikiwa ni baada ya kuiwasilisha Bungeni.
Amesema watu hao wamepata tiba kwenye vitengo vya afya ya akili katika hospitali za rufaa za mikoa na kanda,kliniki za MAT na nyumba za upataji nafuu sober house nchini
Amesema kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa kipindi cha mwaka 2025, makosa ya dawa za kulevya mashauri 1124 yalifunguliwa katika Mahakama mbalimbali nchini na mashauri 1373 yalitolewa hukumu na Jamhuri ikishinda mashauri 1058.
Amesema mali zenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 3.3 zilizohusishwa na makosa ya dawa za kulevya zilitaifishwa.
Amesema mwaka 2025 jumla ya tani 1,074.72 za dawa za kulevya zilikamatwa katika operesheni zilizofanyika katika maeneo mbalimbali nchini,dawa hizo zinajumuisha bangi tani 1,014.06, mirungi tani 26.36,skanka tani 3.20,kratom tani 29.52,heroine kilogram 672.23,cocaine kilogram 4.89,methamphetamine kilogram 907.18,MDA grams 7.82 na MDMA gram 178.
Amesema bangi imeendelea kukamatwa kwa wingi na kwamba kiasi kilichokamatwa kilipungua kwa asilimia 55.97 ikilinganishwa na mwaka 2024, hiyo ni kutokana na uteketezaji wa mashamba ya bangi uliofanyika 2024,kuimarika kwa udhibiti ikiwemo utoaji elimu kwa jamii inayojihusisha na ki,imo cha bangi kuhusu madhara ya kilimo cha zao hilo.

Profesa Kabudi amesema mirungi ilifuatia katika dawa za kulevya zilizokamatwa ambapo jumla ya tani 26.36 zilikamatwa,kiasi hicho kiliongezeka kwa asilimia 42.88 ikilinganaishwa na mwaka 2024,ongezeko hilo linaashiria kuimarika kwa operesheni za ufuatiliaji na udhibiti hususan katika maeneo ya mipaka na njia zinazotumika kusafirisha dawa hizo.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali, Mamlaka Ya Kudhibiti Na Kupambana Na Dawa Za Kulevya Aretas Lyimo amesema katika kuimarisha mapambano dhidi ya dawa hizo, Mamlaka imepanga kufungua ofisi katika mikoa mbalimbali ikianza na mkoa wa Morogoro ambao kwa sasa ndio kinara wa kilimo cha bangi ukifuatia Tabora na Mara.

Kuhusu dawa nyingine za kulevya amesema miaka ya hivi karibuni kumeibuka uingizaji wa dawa ngeni za kulevya nchini ambazo pamoja na Methylenedioxyamphetamine (MDA) na Methylenedioxymethamphetamine (MDA).
Amesema dawa hizo hutengenezwa kwa kutumia kemikali bashrifu pekee ambapo mwaka 2025 kiais cha gram 7.82 za MDA namgramu 178 za MDMA zilikamatwa.,425

