MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: NIDA Kufanya Usajili Wa Watoto  Kuanzia Umri Wa Kuzaliwa,Kutoa Namba Maalum
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > NIDA Kufanya Usajili Wa Watoto  Kuanzia Umri Wa Kuzaliwa,Kutoa Namba Maalum
Habari

NIDA Kufanya Usajili Wa Watoto  Kuanzia Umri Wa Kuzaliwa,Kutoa Namba Maalum

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Lucy Lyatuu,Dodoma
SERIKALI  imesema licha ya kusogeza huduma za ugawaji wa vitambulisho karibu na wananchi, na kuanzisha huduma ya kutuma ujumbe mfupi kwa wananchi ambao vitambulisho vyao vimechapishwa kuwataka kufika katika ofisi za wilaya walizojisajili na kuvichukua, bado kuna vitambulisho 668,822 katika ofisi za wilaya za NIDA ambavyo havijachukuliwa.
 Aidha, imesema   NIDA inatarajia kuanza kufanya usajili wa watoto kuanzia umri wa kuzaliwa ili kutoa namba ya utambulisho ya kipekee ambayo itajulikana kama JAMII NAMBA.
 Waziri wa Mambo Ya Ndani Ya Nchi, Patrobas Katambi amesema hayo wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo Bungeni na kuongeza kuwa NIDA imeanzisha namba maalum ya kutuma ujumbe mfupi bila malipo (sms) ambayo ni 15274.
Habari Picha 12205
Amesema wananchi wote waliopewa taarifa ya kuchukua vitambulisho vyao kujitokeza kwenda kuvichukua kwa kuwa vitambulisho hivyo vitawawezesha kupata utambulisho rasmi katika kupata huduma mbalimbali za kijami, kiuchumi na kiusalama ikiwemo Bima ya Afya,
“Namba hiyo itamuwezesha mwananchi kufuatilia hatua ya maombi ya kitambulisho cha Taifa ilipofikia pamoja na kupata namba yake ya utambulisho bila kulazimika kufika katika ofisi za NIDA,” amesema na kuwataka  Wabunge kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao kutumia namba 15274 kupitia simu.
Amesema katika kuhakikisha NIDA inakuwa na kanzidata yenye taarifa sahihi za watu, Serikali imetoa kibali maalumu cha mwaka mmoja kuanzia mwezi Oktoba 2025 hadi Septemba 2026 cha kuruhusu wananchi waliotoa taarifa zisizo sahihi wakati wa usajili, kufanya mabadiliko ya taarifa hizo na kutoa taarifa sahihi.
Amesema hadi kufikia Aprili 2026 NIDA imepokea na kufanyia kazi maombi ya mabadiliko ya taarifa kutoka kwa wananchi 873 na kutoa rai kwa wananchi wenye changamoto ya taarifa zao katika mfumo wa NIDA kutumia fursa iliyotolewa ya kufanya maboresho ya taarifa zao na kuhakikisha taarifa wanazotoa ni sahihi.
 Kuhusu namba kwa watoto amesema NIDA inatarajia kuanza kufanya usajili wa watoto kuanzia umri wa kuzaliwa ili kutoa namba ya utambulisho ya kipekee ambayo itajulikana kama JAMII NAMBA.
Amesema namba hiyo itatumika katika kupatiwa huduma mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kiusalama tangu mtu anapozaliwa hadi mwisho wa maisha yake.

You Might Also Like

Bonifas Jacob aahidi  akishinda Uenyekiti Kanda ya Pwani hatakaa ofisini

Mume na Mke Wafariki Kwa Wivu Wa Kimapenzi

BRAC Tanzania: Upo Umuhimu Sekta Binafsi, Serikali Kushirikiana

Taasisi za Elimu Geita Zatakiwa Kuanza Programu ya Maziwa Shuleni

BUWSSA Yapewa Bilioni 28 Kutatua Tatizo La Maji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA Yatumia Mbinu za Kibaiolojia Kudhibiti Gugu Ziwa Victoria
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TPHPA Yatumia Mbinu za Kibaiolojia Kudhibiti Gugu Ziwa Victoria
Habari May 24, 2026
Wizara Ya Viwanda Kutekeleza Vipaumbele Saba, Ipo  Miradi Ya Viwanda Ya  Kimkakati
Habari May 22, 2026
Biashara 15 Hazitakiwi Kufanywa Na Wageni Ndani Ya Nchi
Habari May 22, 2026
Wadau wataka mifumo jumuishi kupunguza mzigo wa malezi kwa wenye ulemavu
Habari May 21, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?