MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: MAIPAC NA THRDC Watoa Mafunzo Kwa Waandishi Wa Habari Za Mazingira, Kanda Ya Ziwa
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > MAIPAC NA THRDC Watoa Mafunzo Kwa Waandishi Wa Habari Za Mazingira, Kanda Ya Ziwa
Habari

MAIPAC NA THRDC Watoa Mafunzo Kwa Waandishi Wa Habari Za Mazingira, Kanda Ya Ziwa

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Mwandishi Wetu
MWANZA: TAASISI  ya Wanahabari ya Usaidizi kwa Jamii za Pembezoni (MAIPAC) kwa kushirikiana na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) wamezindua mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari za mazingira wa Kanda ya Ziwa, yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika kwa weledi pamoja na kuwasaidia kuelewa sheria mbalimbali zinazohusiana na mazingira.
Mafunzo hayo yanahusisha waandishi wa habari 35 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, na ni sehemu ya utekelezaji wa programu endelevu inayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Kabla ya mafunzo hayo, awamu ya kwanza iliwahusisha waandishi wa habari kutoka Kanda ya Kaskazini.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Miradi wa THRDC, Wakili Halima Sonda, amewataka waandishi wa habari kuzingatia uandishi wa habari za kiuchunguzi zinazohusu mazingira ili kusaidia jamii kupata taarifa sahihi na kuchukua hatua dhidi ya changamoto za kimazingira.
Amesema jamii zimekuwa zikiathirika kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira, hivyo vyombo vya habari vina jukumu muhimu la kuelimisha umma na kusaidia kupunguza athari hizo kupitia taarifa za kitaaluma na zenye ushawishi.
Habari Picha 12149
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa MAIPAC, Mussa Juma Siwayombe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wafanyakazi katika Vyombo vya Habari (JOWUTA), amewataka wanahabari kufahamu vyanzo vya uharibifu wa mazingira na mbinu za kukabiliana navyo.
Amesema uandishi wa habari za mazingira unahusisha maeneo mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira, ukame, uhifadhi wa wanyamapori, kilimo pamoja na mipango bora ya matumizi ya ardhi.
Siwayombe amesisitiza kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wanahabari kuandika habari za kina na za kiuchunguzi zitakazosaidia kuibua changamoto za mazingira, kushawishi maboresho ya sera na sheria, na hatimaye kulinda jamii zinazoathirika.
“MAIPAC na THRDC tutaendelea kuwasaidia ili mtimize wajibu wenu. Tunataka kuona matokeo chanya kutoka kwenye mafunzo haya,” amesema.
Naye Wakili Paul Kisabo alipokuwa akitoa mada kuhusu sheria zinazosimamia masuala ya mazingira, amewataka wanahabari kuzifahamu sheria hizo ili kuimarisha weledi katika kazi zao na kuepuka changamoto za kisheria.
Pia amewahakikishia wanahabari kuwa wataendelea kupata msaada wa kisheria pale wanapokumbana na changamoto za kikazi, hususan katika uandishi wa habari za kiuchunguzi na masuala ya maslahi ya umma.
Mwanahabari mkongwe, Edwin Soko, amewataka washiriki kutambua jukumu lao kubwa la kuwa sauti ya wasio na sauti katika jamii, hususan katika masuala yanayohusu ulinzi wa mazingira.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuendelea katika kanda nyingine nchini, yakiwa na lengo la kuongeza wigo wa uelewa kwa wanahabari kuhusu uandishi wa habari za mazingira na sheria zake.

You Might Also Like

Tafiti Nguzo Ya Maendeleo Ya Biashara, Uchumi – Katambi

Matumizi Holela Ya Vilevi Hatari Kwa Watumiaji

Jaffo Aagiza Kufufuliwa Vilivyokuwa Viwanda Vya Serikali

Watu Wenye Ulemavu Nchini Wafikia Mil 5.3

Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TPHPA Yaendelea Kutoa Elimu YA Matumizi Salama Ya Viuatilifu
Next Article Wizara ya Maji: Uhifadhi Ziwa Victoria Unahitaji Ushirikiano, Uwekezaji Endelevu
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Wizara ya Maji: Uhifadhi Ziwa Victoria Unahitaji Ushirikiano, Uwekezaji Endelevu
Habari May 20, 2026
TPHPA Yaendelea Kutoa Elimu YA Matumizi Salama Ya Viuatilifu
Habari May 20, 2026
Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Yasisitiza Uhifadhi
Habari May 20, 2026
Tunashauri Ufugaji wa Samaki Kwenye Vizimba, Mavuno ni Mengi – TAFIRI
Habari May 20, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?