MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti
Habari

IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Kilimo cha Maeneo ya Tropiki (IITA), Dkt. Simeon Ehui amesema Afrika inapaswa kuongeza uzalishaji wa chakula ili kukidhi ongezeko kubwa la watu huku ikiendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa ardhi na hali ngumu za kiuchumi.
Dk. Ehui amesema hayo katika hafla ya kutafakari ushirikiano kati ya IITA na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo amesisitiza kuwa mustakabali wa kilimo barani Afrika hautategemea rasilimali pekee, bali ushirikiano wa karibu kati ya serikali, taasisi za utafiti, sekta binafsi, vijana wabunifu na wakulima.
Amesema katika kipindi cha miaka 12 iliyopita, IITA imewekeza takribani Sh bilioni 410.75 nchini Tanzania, sawa na dola za Marekani milioni 154.57, kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya kilimo na utafiti.
Habari Picha 12014
Kwa mujibu wa Dkt. Ehui, kati ya fedha hizo Sh. Bilioni 318.88 zimeelekezwa katika shughuli za utafiti, huku sehemu ya fedha hizo ikipelekwa kwa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) pamoja na vyuo vikuu vya ndani.
Aidha, Sh. Bilioni 53.68 zimetumika kulipa mishahara ya wafanyakazi wazawa na Sh. Bilioni 38.19 kuwekeza katika miundombinu na vifaa.
Amesema taasisi hiyo pia imewekeza katika maendeleo ya rasilimali watu kwa kufadhili wanafunzi 60 wa shahada za uzamivu na wanafunzi 80 wa shahada za uzamili, pamoja na kutoa mafunzo kwa zaidi ya vijana 10,000 na wakulima zaidi ya 11,000.
“Nyuma ya takwimu hizi kuna maisha yaliyobadilika, vijana waliowezeshwa na matumaini mapya kwa jamii za wakulima,” amesema.
Habari Picha 12013
Dkt. Ehui ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake wa muda mrefu na kumpongeza Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kuimarisha uwepo wa IITA nchini tangu mwaka 2013.

You Might Also Like

Utafiti Wa Roketi UDOM Uko Mbioni Kukamilika

Wizara Yapanga Kunufaika Na Maarifa Ya Mabalozi Wastaafu

CMSA Yatoa Elimu ya Uwekezaji kwa Wananchi na Wakulima Nanenane

Mwalim Ahaidi Kubadilisha Dodoma Kuwa Jiji Kamili La Makao Makuu

Dkt. Majule Ahoji Hatua za Kulinda Wananchi Dhidi ya Mikopo Hatari

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Vyuo Vikuu Vyahitaji Mkakati Madhubuti wa Tafiti — Yanda
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vyuo Vikuu Vyahitaji Mkakati Madhubuti wa Tafiti — Yanda
Habari May 8, 2026
Asilimia 26 Ya Wanawake Ndio Wanaoamini Kuwa Na Uhuru Wa Kufanya Maamuzi Ya Kufanya Shughuli Za Uchumi
Habari May 8, 2026
Kesi 100 Za Wananchi Zasikilizwa Na Kupatiwa Suluhu Katiba Na Sheria
Habari May 8, 2026
Wizara Ya Elimu Yaomba Kuidhinishiwa Trilioni 2.3
Habari May 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?