MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Vyuo Vikuu Vyahitaji Mkakati Madhubuti wa Tafiti — Yanda
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Vyuo Vikuu Vyahitaji Mkakati Madhubuti wa Tafiti — Yanda
Habari

Vyuo Vikuu Vyahitaji Mkakati Madhubuti wa Tafiti — Yanda

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
MBUNGE wa Buhigwe mkoani Kigoma, Profesa Pius Yanda, ameishauri Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuongeza bajeti ya tafiti katika vyuo vikuu ili kuviwezesha taasisi hizo kutoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya taifa.
Profesa Yanda ametoa ushauri huo bungeni alipokuwa akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akisema uwekezaji wa kutosha katika utafiti utaviwezesha vyuo vikuu kushindana kimataifa na kuzalisha maarifa yenye tija kwa jamii.
Amesema kwa miaka iliyopita vyuo vikuu vilikuwa vikisaidiwa na serikali pamoja na washirika wa maendeleo katika shughuli za utafiti, lakini bado kuna haja ya kuweka mkakati thabiti wa kuhakikisha eneo hilo linaimarishwa zaidi.
Aidha, Profesa Yanda ameeleza kuwa ongezeko la wanafunzi katika ngazi mbalimbali limeongeza mzigo kwa wahadhiri, hali inayopunguza muda wa kufanya tafiti.
Amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kuajiri wahadhiri wapya, hatua inayosaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa watumishi vyuoni.
Hata hivyo, amesisitiza umuhimu wa kuzingatia miongozo ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) katika ajira hizo, akibainisha kuwa uwiano wa wahadhiri wakongwe na vijana ni muhimu katika kuimarisha ubora wa elimu na utafiti.
Profesa Yanda amesema vyuo vikuu havipaswi kujikita katika ufundishaji pekee, bali pia kufanya tafiti zitakazosaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Ameongeza kuwa ameshiriki katika maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kupitia timu ya wataalamu waliokuwa wakichakata taarifa na kutoa mapendekezo ya kitaalamu.
Pia ameshauri Tanzania kuiga mifumo ya baadhi ya nchi za Afrika zinazotumia wataalamu kuchambua taarifa za maendeleo kila baada ya miaka mitano ili kuboresha mipango ya maendeleo ya taifa.

You Might Also Like

Yonaz akabidhi boti ya doria kukabili vitendo vya kiuhalifu

Ulega: Miaka 50 ya ILRI imeinufaisha Tanzania 

Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano

Afrika ijadili changamoto sekta ya utalii – UN

NSSF Kutoa Mafao Siku Moja Baada ya Kustaafu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Asilimia 26 Ya Wanawake Ndio Wanaoamini Kuwa Na Uhuru Wa Kufanya Maamuzi Ya Kufanya Shughuli Za Uchumi
Next Article IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti
Habari May 9, 2026
Asilimia 26 Ya Wanawake Ndio Wanaoamini Kuwa Na Uhuru Wa Kufanya Maamuzi Ya Kufanya Shughuli Za Uchumi
Habari May 8, 2026
Kesi 100 Za Wananchi Zasikilizwa Na Kupatiwa Suluhu Katiba Na Sheria
Habari May 8, 2026
Wizara Ya Elimu Yaomba Kuidhinishiwa Trilioni 2.3
Habari May 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?