MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua
Habari

Mbunge Msita Ataka Ukarabati Wa Haraka Barabara Zilizoharibiwa Na Mvua

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: SERIKALI imeshauriwa kuongeza uwekezaji katika miundombinu ya barabara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kupunguza ajali zinazotokana na ubovu wa barabara nchini.
Ushauri huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Itigi, John Msita, alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni jijini Dodoma.
Msita amesema maendeleo ya uchumi wa kati wa juu hayawezi kufikiwa bila uwepo wa mtandao imara wa barabara zinazopitika wakati wote, akisisitiza kuwa miundombinu hiyo ni mhimili muhimu wa maendeleo ya Taifa.
Ameeleza kuwa mvua zinazoendelea kunyesha zimeharibu kwa kiasi kikubwa barabara nyingi za lami zinazohudumiwa na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), hali inayochangia ongezeko la ajali za barabarani, hususan za mabasi, zinazosababisha vifo na majeruhi.
“Tunashuhudia mafuriko yakiharibu barabara na kusababisha ajali kutokana na mashimo na uharibifu wa miundombinu. Ni muhimu Serikali ichukue hatua za haraka kufanya ukarabati ili barabara ziweze kupitika wakati wote,” amesema.
Akizungumzia umuhimu wa barabara katika uchumi, Msita ameitaja barabara ya Mkiwa–Itigi–Mitundu–Rungwa hadi Makongorosi (Chunya) kuwa kiungo muhimu kinachounganisha mikoa ya Songwe, Mbeya, Tabora, Singida na Dodoma, pamoja na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kutoka nchi jirani za Zambia na Malawi.
Amesema kuchelewa kukamilika kwa barabara hiyo kunakwamisha jitihada za kukuza uchumi na kufikia malengo ya maendeleo ya muda mrefu, akisisitiza kuwa barabara bora ni msingi wa ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Katika hoja nyingine, Mbunge huyo ameeleza kuwa sehemu kubwa ya mtandao wa barabara nchini unasimamiwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ambapo nyingi ni za udongo na huathirika zaidi wakati wa mvua.
Kutokana na hali hiyo, ametoa wito kwa wabunge kushinikiza kuongezwa kwa bajeti ya TARURA ili kuboresha barabara hizo na kuhakikisha zinapitika kwa urahisi mwaka mzima.
Aidha, Msita amezungumzia changamoto za matumizi ya ardhi katika Wilaya ya Manyoni, akibainisha kuwa uwepo wa mapori ya akiba ya Rungwa, Muhesi na Kizigo unazuia wananchi kupanua shughuli za kiuchumi licha ya uwepo wa rasilimali nyingi.
Amependekeza Serikali ipitie mipaka ya mapori hayo kwa kuyapunguza ili kutoa nafasi kwa wananchi kufanya kilimo na ufugaji, akieleza kuwa ongezeko la watu limeongeza mahitaji ya ardhi.
Pia amegusia changamoto za upatikanaji wa vitambulisho vya Taifa na vyeti vya kuzaliwa, akisema wananchi wengi vijijini hukumbana na matatizo ya mtandao wanapofuatilia huduma hizo.
Ameitaka Serikali kuboresha mifumo ya utoaji huduma hizo ili kupunguza usumbufu kwa wananchi na kuimarisha uwazi katika upatikanaji wake.

You Might Also Like

Serikali Yaweka Utaratibu Biashara Pembezoni mwa Barabara

Geita Ina Dhahabu Lakini Haina Maendeleo” – Salum Mwalim

Daktari: Saratani ya Matiti Inazuilika, Inatibika

Mashine Kusaidia Uuzaji Vinywaji Bila Muuzaji

Serikali Yasema Migogoro Ya Ndoa lliyotatuliwa Imeongezeka

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Mbunge Ndoinyo Aitaka Serikali Kugawa Ngorongoro Kusogeza Huduma Karibu
Next Article Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ubunifu Wa Majengo Watakiwa Kuzingatia Tija Na Gharama Nafuu
Habari April 11, 2026
Waziri Ulega aridhishwa na miradi ya dharura TANROADS
Habari April 11, 2026
Mbunge Majule ataka wanawake wapewe elimu ya fedha na mitaji
Habari April 11, 2026
Mbunge Ndoinyo Aitaka Serikali Kugawa Ngorongoro Kusogeza Huduma Karibu
Habari April 10, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?