MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: EAC Yaweka Mguu Chini Ushirikishwaji Wa Wanawake Katika Amani, Ulinzi Na Usalama
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > EAC Yaweka Mguu Chini Ushirikishwaji Wa Wanawake Katika Amani, Ulinzi Na Usalama
Habari

EAC Yaweka Mguu Chini Ushirikishwaji Wa Wanawake Katika Amani, Ulinzi Na Usalama

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MKUTANO  wa 13 wa Pamoja wa Mabaraza ya Kisekta ya Mawaziri wa Ushirikiano katika Ulinzi, Amani na Usalama na Baraza la Kisekta la Uratibu wa Sera za Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umehitimishwa  jijini Nairobi, Kenya na kuweka bayana vipaumbele vya Jumuiya katika Mabaraza hayo.
Ushirikishwaji wa Wanawake katika masuala ya amani, ulinzi na usalama ni kati ya ajenda zilizojadiliwa na kufanyiwa maamuzi ambapo Jumuiya imepitisha Mpango Mkakati wa kwenda sambamba na wanawake katika ulingo huo. Ajenda hiyo pia ni Utekelezaji wa Azimio la Baraza la Usalama la  1325 (UNSCR 1325) la Umoja wa Mataifa.
EAC pia imejadili kuanzishwa kwa mfumo jumuishi wa tahadhari za mapema katika masuala ya ulinzi, usalama na majanga .
Habari Picha 11668
Aidha, katika kuhakikisha Mfumo wa Jumuiya wa uzuiaji na utatuzi wa migogoro unakuwa na tija, mkutano huu umepitisha Mpango Mkakati wa Ushirishwaji wa Asasi zisizo za kiserikali ili kutekeleza msingi wa ujumuishwaji wa wananchi katika shughuli za kikanda.
Mkutano huo ulioongozwa na Mwenyekiti, Makamu wa Kwanza wa Waziri Mkuu na Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Rebecca Kadaga kutoka Jamhuri ya Uganda umesisitiza umuhimu wa kuharakisha utekelezaji wa uamuzi na maelekezo yanayotolewa na Mabaraza hayo na kuratibu vyema sera za mambo ya nje ili kukabiliana na changamoto zinazoibuka za usalama na mabadiliko ya kisiasa duniani.
Ajenda zilizojadiliwa zinaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 huku Tanzania ikiwa tayari imeanza utekelezaji wa ndani wa ajenda hizo ikiwemo kuwa na viongozi mahiri na shupavu wanawake katika sekta za ulinzi na usalama.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Patrobas Katambi , akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki Balozi Said Shaib Mussa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Maduhu Kazi.

You Might Also Like

Profesa Ndunguru: Teknolojia ya Vinasaba Yafungua Ukurasa Mpya Katika Kilimo

Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza

Mafunzo ya Ufundi Sasa Kupatikana Popote Kupitia Programu ya VSOMO”

Tume ya umwagiliaji yapambana kuinua kilimo

Mgombea NCCR-Mageuzi Awaasa Watanzania Wasikubali Propaganda

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kila Parachichi, Ndizi au Chungwa Ninalouza ni Tiketi Ya Matumaini Ya Watoto Wangu – Beatrice
Next Article TAWIA na MAIPAC washirikiana kuadhimisha Siku ya Wajane, wapanga kupanda Mlima Kilimanjaro
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

VETA kumpa nafasi Igobeko kuongeza ujuzi na kuwawezesha wengine
Habari August 23, 2026
Airtel Yajenga Darasa La Fursa Katika Shule Ya Sekondari Magaoni,Tanga
Habari August 23, 2026
Bunifu ya dawa ya mayai yapunguza hasara kwa wafugaji wa kuku
Makala August 22, 2026
Dkt Yonaz Awakumbusha Vijana Kulinda Afya Zao Katika Mapambano Dhidi Ya Ukimwi
Habari August 22, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?