MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: TEEA YAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MADINI KUIMARISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > TEEA YAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MADINI KUIMARISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Habari

TEEA YAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MADINI KUIMARISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na mwandishi wetu , Dodoma
TAASISI  ya Wataalamu wa Mazingira Tanzania (TEEA) imeomba kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Madini ili kuhakikisha shughuli zote za utafutaji, uchimbaji na uchakataji wa madini nchini zinafanyika kwa kuzingatia misingi ya utunzaji na uendelezaji wa mazingira.
Ombi hilo limetolewa April mosi mwaka huu, 2026
 katika ofisi za Wizara ya Madini zilizopo Mtumba jijini Dodoma, ambapo uongozi wa taasisi hiyo umefanya kikao na baadhi ya maofisa wa wizara hiyo kujadili namna bora ya kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za kimazingira.
Katika kikao hicho, viongozi wa TEEA walitaja maeneo yanayochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kuwa ni pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji, uharibifu wa ardhi unaotokana na uchimbaji holela, ukataji wa miti bila udhibiti, pamoja na matumizi ya kemikali hatarishi kama zebaki katika shughuli za uchimbaji mdogo.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Emmanuel Hanai amesema ushirikiano kati ya TEEA na Wizara ya Madini utatoa fursa pana kwa watumishi wa wizara hiyo kuongeza uelewa, maarifa na ujuzi kuhusu mbinu bora za uhifadhi wa mazingira, sambamba na kuimarisha utekelezaji wa sera na miongozo ya kimazingira.
Ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017, TEEA imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) pamoja na taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali katika kuhamasisha na kusimamia masuala ya uhifadhi wa mazingira nchini.
“Kwa kuzingatia viwango bora vya kimazingira, tunaweza kuongeza thamani ya madini yetu na kuvutia uwekezaji zaidi, hali itakayowezesha sekta hii kuchangia mapato ya dola za Marekani kati ya  milioni 50 hadi 100 kwa mwaka,” amesema Hanai.
Kwa upande wake, Kaimu Kamishna wa Madini,  Elias Kayandabila ameipongeza TEEA kwa wazo hilo, na amesema ni hatua muhimu itakayosaidia kuongeza ufanisi wa watumishi wa wizara hiyo, hususan wale wanaoshughulikia masuala ya mazingira moja kwa moja.

You Might Also Like

TEA Yatathmini Utekelezaji na Kupanga Mwelekeo Mpya Kupitia Baraza la Wafanyakazi

Kamati Ya Bunge Yakagua Mradi Wa Nyumba NSSF

Mbunge Ulanga Aweka Mikakati Kuufungua Mkoa wa Morogoro Kimaendeleo

Rais Dk Mwinyi Kukata Keki Sabasaba

Serikali Kuanzisha Kituo Maalum Cha Kuwezesha Wawekezaji Vijana

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaendelea Kuimarisha Sekta Ya Utalii, Mapato Yaongezeka
Next Article Kila Parachichi, Ndizi au Chungwa Ninalouza ni Tiketi Ya Matumaini Ya Watoto Wangu – Beatrice
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

TPHPA Yatumia Mbinu za Kibaiolojia Kudhibiti Gugu Ziwa Victoria
Habari May 24, 2026
Wizara Ya Viwanda Kutekeleza Vipaumbele Saba, Ipo  Miradi Ya Viwanda Ya  Kimkakati
Habari May 22, 2026
Biashara 15 Hazitakiwi Kufanywa Na Wageni Ndani Ya Nchi
Habari May 22, 2026
Wadau wataka mifumo jumuishi kupunguza mzigo wa malezi kwa wenye ulemavu
Habari May 21, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?