MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Upotevu Wa Maji Kipimo Cha Utendaji Wa Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Upotevu Wa Maji Kipimo Cha Utendaji Wa Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji
Habari

Upotevu Wa Maji Kipimo Cha Utendaji Wa Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amesema utendaji wa Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Maji utapimwa kwa kuzingatia uwezo wao wa kukabiliana na changamoto hiyo, akisisitiza kuwa suala hilo ni muhimu katika kuongeza ufanisi wa huduma na mapato ya sekta.
Aweso ametoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira kwa mwaka 2024/25, ambapo ameeleza kuwa tathmini iliyofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inapaswa kutumika kuleta mabadiliko ya kweli katika sekta hiyo.
Amesisitiza kuwa ni lazima mamlaka za maji zitatue changamoto ya upotevu wa maji kwa kuwa ni eneo lenye athari kubwa kiuchumi, akieleza kuwa maji yanayopotea ni sawa na fedha inayopotea.
Aidha, Waziri Aweso amehimiza matumizi ya teknolojia za kisasa katika kushughulikia changamoto mbalimbali za sekta, zikiwemo upotevu wa maji, malalamiko ya ankara, pamoja na ulinzi wa miundombinu na vyanzo vya maji.
Habari Picha 11540
Amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za majisafi na usafi wa mazingira kupitia mageuzi ya sekta na usimamizi imara wa mamlaka za maji nchini.
Pia amebainisha umuhimu wa kuwajengea uwezo watendaji wa sekta ya maji ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, pamoja na kuimarisha bodi za wakurugenzi ili kusimamia vyema taasisi hizo na kuhakikisha zinafikia malengo yaliyokusudiwa.
Kadhalika, amesisitiza haja ya kuweka mfumo rasmi wa kisheria utakaowezesha ushirikiano na uwekezaji wa sekta binafsi ili kuongeza ufanisi na rasilimali fedha katika sekta hiyo.
Habari Picha 11541
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mwajuma Waziri, amesema utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan unapaswa kuonekana kwa vitendo kupitia utendaji bora wa mamlaka za maji, akibainisha kuwa maji ni nguzo muhimu ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile, amesema licha ya mafanikio yaliyofikiwa, bado mamlaka za maji zina jukumu kubwa la kuboresha huduma za majisafi na usafi wa mazingira, huku akisisitiza uwajibikaji wa wakurugenzi watendaji katika usimamizi wa rasilimali watu, fedha na utekelezaji wa mipango ya taasisi kila mwaka.
Habari Picha 11542
Kwa ujumla, tathmini ya utendaji inaonesha dhamira ya Serikali ya kuhakikisha mamlaka zote za maji zinatoa huduma bora kwa kuzingatia ufanisi, uwajibikaji na matumizi sahihi ya rasilimali, huku mafanikio ya sekta yakipimwa kwa namna yanavyogusa maisha ya wananchi kupitia huduma bora, salama na endelevu.

You Might Also Like

HATUNA HURUMA NA WADANGANYIFU KWENYE MITIHANI – WAZIRI MKENDA

Silaa Atembelea Banda La NEMC, Wiki Ya Anwani Za Makazi

Dkt. Biteko Aahidi Kuendeleza Miradi Mikubwa Bugelenga

Katambi Aitaka TIRDO Kuongoza Mapinduzi ya Kufufua Viwanda Nchini

WDC Kuboresha Miradi Yake Ya Majengo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Walimu Ni Nguzo ya Maadili na Uzalendo kwa Taifa – Rais CWT
Next Article Dkt. Nchimbi Azindua Mfumo Mpya wa Utabiri wa Kiasi cha Maji Morogoro
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

IITA Yawekeza Bilioni 410 Tanzania Kuimarisha Kilimo, Utafiti
Habari May 9, 2026
Vyuo Vikuu Vyahitaji Mkakati Madhubuti wa Tafiti — Yanda
Habari May 8, 2026
Asilimia 26 Ya Wanawake Ndio Wanaoamini Kuwa Na Uhuru Wa Kufanya Maamuzi Ya Kufanya Shughuli Za Uchumi
Habari May 8, 2026
Kesi 100 Za Wananchi Zasikilizwa Na Kupatiwa Suluhu Katiba Na Sheria
Habari May 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?