MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Walimu Ni Nguzo ya Maadili na Uzalendo kwa Taifa – Rais CWT
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Walimu Ni Nguzo ya Maadili na Uzalendo kwa Taifa – Rais CWT
Habari

Walimu Ni Nguzo ya Maadili na Uzalendo kwa Taifa – Rais CWT

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
RAIS wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Dkt. Suleiman Ikomba, amesema kuwa nafasi ya mwalimu haijikiti tu kwenye kufundisha darasani, bali pia inahusisha kulea maadili, kujenga uzalendo na kuwa kielelezo bora kwa kizazi kijacho.
Akizungumza katika mahojiano maalum, Dkt. Ikomba ameeleza kuwa jukumu la mwalimu linazidi mipaka ya maandalizi ya masomo, kwani linahusisha kujenga jamii yenye nidhamu, utu na uwajibikaji.
Akizungumzia mchango wa CWT, amesema chama hicho kinaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha walimu wanadumisha hadhi ya kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
Amefafanua kuwa, chama kinaweka mkazo katika kuimarisha maadili ya taaluma ya ualimu kupitia mikutano, semina na majadiliano ya kitaaluma kwa wanachama wake, ili kuwakumbusha wajibu wao kwa wanafunzi, jamii na taifa.
Aidha, amebainisha kuwa CWT inashirikiana na mamlaka husika kukuza taaluma ya walimu, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wao katika kufundisha na kulea kwa weledi zaidi.
Pia amesisitiza umuhimu wa walimu kuzingatia uwajibikaji na nidhamu ya kazi, akieleza kuwa mwalimu mwenye maadili na ujuzi wa hali ya juu huwa kielelezo cha jamii nzima.
Dkt. Ikomba amehitimisha kwa kusisitiza kuwa lengo kuu la chama hicho ni kuhakikisha mwalimu wa Tanzania anapata heshima stahiki, anawajibika ipasavyo na anakuwa mfano bora kwa wanafunzi pamoja na jamii kwa ujumla.

You Might Also Like

Maadhimisho Ya VETA Ya Miaka 30 Kuhitimishwa Machi 18 Hadi 21, DSM

Profesa Anangisye Atoa Neno Kwa Wahitimu

Katibu Mkuu CCM Dkt. Nchimbi Akutana na Katibu Mkuu CRC

Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050

Serikali yatambua deni la Kiwira Coal Mine Bill.1.52

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Uwekezaji wa NSSF wa Mzizima Towers Kufungua Fursa Mpya za Biashara na Utalii Dar
Next Article Upotevu Wa Maji Kipimo Cha Utendaji Wa Wakurugenzi Wa Mamlaka Za Maji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

VETA  Yapongezwa Kwa Kuibua Vipaji Kwa Vijana  
Habari June 24, 2026
Kundi Kubwa La Wanafunzi Hukatisha Masomo Katika Ngazi Mbalimbali Ya Elimu -TEWW 
Habari June 24, 2026
TEMESA  Yajadhimisha Miaka 20, Yajivunia  Mafanikio  Na Kuahidi  Kuimarisha  Huduma
Habari June 24, 2026
PURA Yasema Tanzania Inaendelea Kujivunia Uwepo Wa Gesi Asilia,Ni Nguzo Muhimu Katika Kuchochea Maendeleo
Habari June 24, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?