MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Dawati  La Jinsia Unguja Latoa Ulinzi Na Usalama Kwa Watoto Wa Kike Kuwaepusha Na Ukatili
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Dawati  La Jinsia Unguja Latoa Ulinzi Na Usalama Kwa Watoto Wa Kike Kuwaepusha Na Ukatili
Habari

Dawati  La Jinsia Unguja Latoa Ulinzi Na Usalama Kwa Watoto Wa Kike Kuwaepusha Na Ukatili

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Lucy Lyatuu
 DAWATI  la Jinsia na Watoto la Polisi lililopo Madema, Unguja, likiungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA)  Kwa
pamoja na Serikali ya Finland limetoa ulinzi na kuhakikisha usalama Kwa makundi ya watoto wa kike katika eneo hilo Kwa kuwaepusha na ukatili wa ndoa za utotoni.
Hatua hiyo imewezesha miongoni mwa watoto wa kike kutimiza ndoto zao,lakini pia wazazi wakiwezeshwa kushiriki mijadala elekezi iliyolenga kushughulikia mila na mitazamo inayochochea ndoa za utotoni.
Akitoa ushuhuda katika maadhimisho ya siku ya mwanamke, Zuhra  (ambaye sio jina halisi) amesema elimu yake ilitarajiwa kukatishwa, utoto wake ungeisha ghafl kama ilivyo kwa wasichana wengi wanaokabiliwa na ndoa za utotoni.
Amesema alipokuwa na umri wa miaka 17 , mustakabali wake ulikuwa unaamuliwa na wengine.
“Sikuwa na uwezo mkubwa wa kupinga mpaka pale hatua moja muhimu ilipobadilisha kila kitu,” amesema na kuongea kuwa msaada huo haukumhusu Zuhra pekee bali na wazazi.
 Amesema kupitia mchakato huo, familia ilifanya uamuzi mkubwa uliobadilisha maisha, ndoa iliyokuwa imepangwa ilifutwa, mahari ilirejeshwa, na wazazi wote wawili wakajitolea kuhakikisha watoto wao wote wanaendelea na masomo.
Amesema Baada ya kuondokana na tishio la ndoa ya utotoni, alirejea shuleni akiwa na ari mpya na Kwa sasa amemaliza elimu yake ya sekondari na anaendelea na masomo zaidi katika fani ya sheria.
Amesema ndoto yake ni kufanya kazi na wanawake na wasichana waliokumbwa na ukatili wa kijinsia na kuhakikisha wengine wanaokabiliwa na hatari kama aliyowahi kukumbana nayo wanapatiwa ulinzi.
“Nataka kuwasaidia wasichana kuelewa haki zao na kujua kwamba ndoto zao zina thamani,” anasema.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, MarkSchreiner  amesema Kuwezesha msichana kutimiza ndoto zake ni moja ya uwekezaji wenye nguvu zaidi wanaoweza kufanya.
 “Kwa ushirikiano na wadau kama Serikali ya Finland, tunabadilisha ulinzi kuwa fursa na kuhakikisha hakuna msichana anayebaki nyuma.”amesema.
Amesema Siku ya Wanawake Duniani inakumbusha kwamba wasichana wanapopewa nafasi ya kudai haki zao na kufanya maamuzi yao wenyewe, jamii nzima inasogea karibu zaidi na usawa na haki.
Baba wa Zuhra, Zimbwe Msumi (jina limebadilishwa), anasema tukio hilo lilibadilisha kabisa uelewa wake kuhusu maana ya kumlinda binti yake.
Nawahimiza wazazi kote Tanzania kusimama kulinda haki za mtoto wa kike, kuwapeleka shule na kuwaunga mkono katika kutimiza ndoto zao. Tunapowalinda wasichana wetu, tunalinda mustakabali wetu.”

You Might Also Like

Ikomba: Aliishi Na Watoto Wiki Sita Akiwafundisha Kabla Ya Mtihani WaTaifa

Rais Samia kufungua kikao kazi cha watendaji serikalini

Wiki ya Huduma za Fedha: SELF Yafungua Fursa za Kiuchumi kwa Wananchi Tanga

TUGHE Yatoa Wito Kwa Wafanyakazi Kujitokeza Kupiga Kura

Kutofuata sheria chanzo kikuu cha migogoro ya kazi – CMA

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia Awekeza Mabilioni Kuboresha Sekta ya Uvuvi
Next Article Tume Ya Madini Yaweka Vipaumbele Kuwezesha Vijana Kushiriki Katika Uchimbaji Madini 
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mwandishi Lucy Ngowi Miongoni mwa Waliong’ara Mei Mosi
Habari May 2, 2026
Tanzania yaendelea kuwa Shule ya Utumishi Barani Afrika,
Habari April 29, 2026
Wizara Ya Kilimo Yaomba Bunge Kuidhinisha Trilioni 1.1,Yaweka Mikakati Kuimarisha Sekta Hiyo
Habari April 28, 2026
NSSF Yafikia Trilioni 11.2, Hifadhi Skimu Yatajwa Kubadili Maisha ya Watanzania
Habari April 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?