MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050
Habari

Serikali Kuwasilisha Bungeni Nyenzo Kuu Tatu Zitakazowezesha Utekelezaji Dira 2050

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu, Dodoma

TUME Ya Taifa Ya Mipango (NPC) kesho jumatatu Februari 2,2026 itawasilisha nyenzo kuu tatu kwa Bunge La Jamhuri Ya Muungano zitakazowezesha kuanza utekelezaji wa Dira 2050.

Aidha Bunge linatakiwa kupokea, kujadili kwa wiki nzima na kufanya uamuzi kwa mujibu wa Katiba.

Nyenzo hizo ni pamoja na mpango elekezi wa muda mrefu yaani wa miaka 25 kuanzia mwaka 2026/2027 hadi mwaka 20250/2051 na Mpango elekezi wa miaka mitano kuanzia mwaka 2026/2027-2030/2031.

Nyenzo nyingine ni mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa wa mwaka 2026/2027 ambazo zitawasilishwa na serikali kupitia Waziri wa Nchi (Mipango na Uwekezaji) Profesa Kitila Mkumbo.

Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Dkt Fred Msemwa amesema hayo jijini hapa wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu maandalizi ya kuanza kwa utekelezaji wa Dira 2050.

Amesema mipango hiyo imepitia ngazi zote za uamuzi serikalini, ambapo itawasilishwa ili kutoa nafasi kwa Bunge kujadili na baadae kufanya maamuzi.

Dkt Msemwa amesema pamoja na nyenzo hizo, Tume imeandaa muongozo utakaohakikisha Mamlaka za serikali za mitaa yakiwemo majiji na Manispaa zote, mikoa yote, Taasisi za umma na Idara na Wizara mbalimbali zinaongozwa vizuri katika kutafsiri na kuelewa mataraji ya Dira 2050 kwa usahihi.

“Kwa msingi huo NPC imeandaa Muongozo wa upangaji wa mipango ya Taifa, ” Amesema Dkt Msemwa na kuongeza kuwa katika kuhakikisba kuwa Muongozo huo unaeleweka baina ya wadau NPC imeshafanya semina na viongozi kutoka Halmashauri zote, Wizara, Idara na Taasisi za umma ili kujadili muongozo huo na kuwa na uelewa wa pamoja.

Amesema katila hatua nyingine NPC ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mfumo wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa tathmini unaolenga kuleta mageuzi ya ufuatiliaji unaozingatia zaidi matokeo ya kazi nanuwajibikaji ambao utaanza kutumika pamoja nanutekelezaji wa Dira 2050 ifikapo Julai 2026.

Kuhusu wananchi kufuatilia uwasilishwaji wa nyenzo hizo, Dkt Msemwa amesema ni muhimu kwa kuwa Dira 2050 imebeba matumaini ya Watanzania na imeandikwa kuzingatia maoni yao, hivyo ni muhimu wananchi kujua na kufuatilia mipango iliyoandaliwa ili kutekeleza Dira yao.

Amesema pia ni fursa ya pekee kwa kila mwananchi kwa kuwa uwasilishwaji wake ni jambo lisilotokea mara kwa mara kwani utatokea tena baada ya miaka 25 ijayo, hivyo ni muhimu wananchi kufuatilia mustakabli wa Taifa lao.

” Dira inasisitiza kuhusu ustawi wa pamoja na ushiriki wa kila mmoja katika ujenzi wa Taifa, Dira ni alama ya umoja na ina nia thabiti ya kutomuacha yeyote nyuma hivyo ni muhimu kila mtanzania kuwa na taarifa kamili ya kinachoendelea katika Mipango ya maendeleo ya Taifa, ” Amesema.

You Might Also Like

CHAUMMA: Tupo Tayari Kupunguza Gharama za Maisha – Salum Mwalim

Mwenyekiti Wa Kijiji Aahidi Kufuatilia Mgogoro wa Shamba Bahi

Mpogolo Aipongeza Halmashauri Maandalizi Mikopo Asilimia 10

Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija

Watu Milioni 300 Afrika Kutumia Nishati Ya Umeme Ifikapi 2030-Biteko

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Yaimarisha Mafunzo Ya Vitendo Kupitia Ushirikiano, Viwanda
Next Article Mbarawa Aitaka Jamii Kulinda Miundombinu ya Uchukuzi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?