MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wanafunzi 571 watunukiwa Stashahada Na Astashaha Za Vyuo Vya Polisi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wanafunzi 571 watunukiwa Stashahada Na Astashaha Za Vyuo Vya Polisi
Habari

Wanafunzi 571 watunukiwa Stashahada Na Astashaha Za Vyuo Vya Polisi

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na  Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM – Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amewatunuku wahitimu 571 waliohitimu mafunzo mbalimbali huku akimshukuru Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake  za kuendeleza na kuimarisha mfumo wa haki jinai nchini  pamoja na kuboresha mafunzo ndani ya Jeshi la Polisi, hali iliyoongeza ufanisi wa utendaji wa jeshi hilo.
IGP Wambura amesema hayo wakati akitunuku stashahada na astashahada kwa wahitimu wa fani mbalimbali katika mahafali ya 10 ya vyuo vya taaluma ya Polisi yaliyofanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA).
Habari Picha 11024
Amesema kupitia uongozi wa Rais Samia, Jeshi la Polisi limepatiwa bajeti ya ununuzi wa vifaa vipya na vya kisasa, utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na maboresho ya mazingira ya kazi, hatua zinazolenga kuimarisha utendaji wa Jeshi la Polisi kwa viwango vya juu zaidi.
Jumla ya wanafunzi 571 walihitimu kutoka vyuo mbalimbali vya Polisi ambavyo ni Polisi Kidatu, Shule ya Polisi Moshi, Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA), Chuo cha Polisi Zanzibar pamoja na Chuo cha Polisi Wanamaji Mwanza.
Habari Picha 11025
Wahitimu hao walipata mafunzo katika fani mbalimbali zikiwemo Stashahada ya Sayansi ya Polisi, Shahada ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Astashahada ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Stashahada ya Sayansi ya Tiba ya Maabara, Astashahada ya Ujuzi wa Usalama Majini pamoja na Ujuzi wa Mawasiliano ya Polisi.
IGP Wambura amewapongeza wahitimu kwa kuamua kujiendeleza kielimu, akisema hatua hiyo haina manufaa kwa Jeshi la Polisi pekee bali pia kwa taifa kwa ujumla. Alisisitiza kuwa elimu ni nyenzo muhimu katika kujenga maadili, weledi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kitaifa.
Habari Picha 11026
“Kuna msemo usemao elimu bora hujenga taifa bora. Elimu ni mwanga unaomwezesha mwanadamu kutambua mema na mabaya,” amesema IGP Wambura huku akinukuu Mithali 4:13 inayosema “Mkamate sana elimu, usimwache aende zake maana yeye ni uzima wako.”
Ameongeza kuwa elimu na mafunzo waliyoyapata wahitimu hao ni hazina isiyo na kipimo itakayowasaidia katika maisha yao ya kitaaluma, kijamii na kiutumishi.
Habari Picha 11027
Aidha, amewataka wakuu wa vyuo vya Polisi kuendelea kuimarisha ushirikiano kupitia mikataba ya makubaliano (MoU) kati ya Jeshi la Polisi na taasisi za elimu ya juu kwa lengo la kuboresha elimu, tafiti na utoaji wa huduma bora kwa jamii.
Amesema ushirikiano huo ni muhimu katika kubadilishana wahadhiri, kusaidiana vifaa vya kujifunzia, kupata fursa za ufadhili, kuimarisha mitandao ya kitaaluma pamoja na kuinua hadhi ya vyuo vya Polisi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti na Mjumbe wa Bodi ya Ushauri na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Profesa Florence Luoga, amewapongeza wahitimu hao akisema kuhitimu katika vyuo vya Polisi ni ishara ya utayari wa kupokea na kutekeleza majukumu mapya kwa weledi na ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Habari Picha 11028
Profesa  Luoga amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuongeza uwezo wa kitaaluma katika vyuo vyake kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kupata ujuzi na taaluma zitakazowasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

You Might Also Like

Rais Samia aweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa Suluhu Sports Academy

NSSF Kutekeleza Mradi Wa Uwekezaji Wa Jengo La Kitega Uchumi Dodoma

MBUNGE wa Kasulu Mjini Ahoji Serikali Kuhusu Mradi wa Maji Mwanga B

October 2, 2024

Massawe Achukua Fomu Kugombea Udiwani Goba

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Elimu Ya Afya, Takwimu sahihi Na Ufuatiliaji Ni Muhimu Kuimarisha Huduma Za Chanjo
Next Article Serikali Yaimarisha Mafunzo Ya Vitendo Kupitia Ushirikiano, Viwanda
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?