MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Elimu Ya Afya, Takwimu sahihi Na Ufuatiliaji Ni Muhimu Kuimarisha Huduma Za Chanjo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Elimu Ya Afya, Takwimu sahihi Na Ufuatiliaji Ni Muhimu Kuimarisha Huduma Za Chanjo
Habari

Elimu Ya Afya, Takwimu sahihi Na Ufuatiliaji Ni Muhimu Kuimarisha Huduma Za Chanjo

Author
By Author
Share
2 Min Read

 

Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI  Msaidizi wa Huduma za Afya kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Dkt. Paul Chaote, amesema kuwa kuimarisha elimu ya afya kwa jamii, matumizi ya takwimu sahihi na ufuatiliaji wa karibu ni msingi wa kuboresha utoaji wa huduma za chanjo nchini.

Amesema kuwa bila vipengele hivyo, juhudi za kufikia watoto wote wanaolengwa haziwezi kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Akihitimisha Mafunzo ya Uongozi wa Kati (Mid-Level Management – MLM)  kuhusu Chanjo  yaliyofanyika Mkoani Iringa, Dkt. Chaote amesema mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha wasimamizi wa huduma za afya kusimamia kwa ufanisi programu za chanjo katika maeneo yao ya kazi.

Habari Picha 11018

“Mafanikio ya huduma za chanjo yanategemea sana usimamizi wa karibu, ufuatiliaji wa mara kwa mara na uwajibikaji katika ngazi zote za utoaji huduma,” amesema Dkt. Chaote.

Aidha, amesema kuwa takwimu sahihi, kamili na kwa wakati ni nyenzo muhimu katika kupanga na kufanya maamuzi sahihi kwenye sekta ya afya.

“Takwimu ndizo dira ya mipango yetu; bila takwimu sahihi hatuwezi kujua tulipotoka, tulipo na tunapokwenda,” amesema, huku akihimiza matumizi sahihi ya taarifa za chanjo katika halmashauri na vituo vya kutolea huduma.

Habari Picha 11019

Pia amesema kuwa kuimarishwa kwa elimu ya afya kwa jamii kuhusu chanjo kutasaidia kuongeza mwitikio wa wananchi na kupunguza imani potofu.

“Jamii ikielewa umuhimu wa chanjo, inakuwa mshirika muhimu katika kulinda afya ya watoto na taifa kwa ujumla,” amesema.

Kwa upande wake, Dkt. Tumaini Haonga, Ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya, amesema mafunzo ya MLM yana mchango mkubwa katika kujenga uwezo wa wasimamizi wa sekta ya afya.

Habari Picha 11020

“Mafunzo haya yanaimarisha uwezo wa kupanga, kufuatilia na kutekeleza programu za chanjo kwa ufanisi zaidi, hasa katika ngazi za halmashauri,” amesema Dkt. Haonga, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya na TAMISEMI.

 

Mafunzo ya MLM yaliyofanyika Mkoani Iringa yamelenga kuimarisha usimamizi wa huduma za chanjo kwa lengo la kuboresha afya ya mama na mtoto, ambapo washiriki wote wa mafunzo walitunukiwa vyeti mara baada ya kukamilisha mafunzo hayo.

You Might Also Like

Ripoti Ya Bodadoda Yazinduliwa

Kamati YA Siasa Yaendelea Kukagua Miradi Ya Maendeleo Temeke

SGR Kipande Cha Saba Na Nane kuanza kujengwa

Mpango Asema Tanzania, Korea Kubadilishana Wafanyakazi

Rais Samia Awateua Tido Mhando, Machumu Na Nyalandu

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article PSPTB Yatangaza Matokeo ya Mitihani ya 32, ,Yawataka Waliokoa Alama Kujisajili Upya 
Next Article Wanafunzi 571 watunukiwa Stashahada Na Astashaha Za Vyuo Vya Polisi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Uwekezaji wa Vijana Watajwa Chachu ya Ukuaji wa Uchumi
Habari June 29, 2026
Tanzania Yaendelea Kuimarisha Usalama Na Ulinzi Wa Taarifa Binafsi
Habari June 29, 2026
WCF Yapigia Debe Ushirikiano na Teknolojia Kuimarisha Hifadhi ya Jamii
Habari June 28, 2026
Sabasaba 2026 Kuingiza Teknolojia Mpya na Fursa za Uwekezaji
Habari June 27, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?