MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Tril.1.5/- Za Umeme Vitongojini: Ndejembi Awasihi Ma-RC Na DC Kusimamia Kwa Ufanisi Mradi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Tril.1.5/- Za Umeme Vitongojini: Ndejembi Awasihi Ma-RC Na DC Kusimamia Kwa Ufanisi Mradi
Habari

Tril.1.5/- Za Umeme Vitongojini: Ndejembi Awasihi Ma-RC Na DC Kusimamia Kwa Ufanisi Mradi

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI  wa Nishati,  Deogratius Ndejembi, amewataka viongozi na watendaji wa ngazi za Mikoa na Wilaya kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Nishati katika kusimamia utekelezaji wa Mradi wa Upelekaji Umeme katika vitongoji 9,009 nchini, ili kuhakikisha unatekelezwa kwa ufanisi na kuwanufaisha wananchi.

Ndejembi ametoa kauli hiyo Januari 22, 2026 jijini Dodoma wakati wa Mkutano Maalum wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa mwaka wa fedha 2024/2025, uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa,  Wakuu wa Wilaya, Waganga Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Lishe wa Mikoa.

Amesema mradi huo unagharimu zaidi ya Sh.trilioni 1.5, fedha zinazotokana na walipa kodi wa Tanzania, hivyo kuna wajibu wa pamoja wa kuhakikisha zinatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia thamani ya fedha

Habari Picha 10900

 

“Mradi huu unatekelezwa kwa fedha za Watanzania, hivyo tuna wajibu mkubwa wa kuusimamia kikamilifu. Mafanikio yake yanategemea ushirikiano wenu kama waratibu wa sekta zote katika maeneo mnayoyasimamia,” amesema Ndejembi.

Aidha, amewakumbusha viongozi hao kutekeleza agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha shule zote, vituo vya afya na zahanati zinafikishiwa umeme kupitia mradi huo, hata kama zipo nje ya umbali wa mita 30 kutoka kwenye miundombinu ya mradi.

Kuhusu gharama za kuunganisha umeme vijijini, Waziri Ndejembi amefafanua kuwa ni sh.27,000 kwa wananchi waliopo ndani ya mita 30 ya mradi, wakati wa utekelezaji na hadi ndani ya miezi mitatu baada ya kukamilika kwa mradi.

Kutokana na hilo, amewataka viongozi wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri kuwahamasisha wananchi kutumia fursa hiyo mapema.

Habari Picha 10901

 

Hata hivyo, ili kuharakisha uunganishaji wa umeme, Waziri Ndejembi ameelekeza kuwa hata  wananchi ambao hawajakamilisha utandazaji wa nyaya katika nyumba zao(partial wiring) waingiziwe umeme bila kusubiri ukamilishaji wa nyumba nzima.

Katika hatua nyingine, amewasisitiza viongozi hao kuzindua miradi ya umeme mara inapokamilika katika maeneo yao bila kusubiri viongozi wa Wizara ya Nishati kufika, ili wananchi waanze kunufaika haraka.

Amesema Wizara ya Nishati inaweka utaratibu madhubuti wa ufuatiliaji wa miradi ya umeme kuanzia ngazi ya Mkoa hadi Wilaya, ili kuhakikisha utekelezaji unakuwa wa ufanisi na kwa viwango vinavyokubalika.

Habari Picha 10902

Pamoja na hayo, amewataka viongozi hao kusaidia kurahisisha upatikanaji wa vibali vya ujenzi wa miradi ya umeme katika maeneo ya misitu, kuhakikisha wakandarasi wanakuwepo kwenye maeneo ya kazi, pamoja na kuwaelimisha wananchi kushirikiana na wakandarasi bila vikwazo na kwamba miradi ya umeme vijijini haina fidia.

Akitoa takwimu za mradi wa umeme vitongojini,  Ndejembi amesema kuwa kati ya vitongoji takribani 64,400 vilivyopo nchini, vitongoji 23,000 vilikuwa bado havijafikiwa na umeme. Kupitia utekelezaji wa mradi wa sasa wa kupeleka umeme katika vitongoji 9,009, vitongoji vitakavyobaki bila umeme vitapungua hadi takribani 13,413 pekee nchi nzima.

Habari Picha 10903

 

Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe.

Habari Picha 10904

 

 

You Might Also Like

Ziara ya Kwanza ya Kiongozi wa Juu wa Tanzania Nchini Belarus Yafungua Ukurasa Mpya wa Ushirikiano

Huduma ya Mahakama ya Mwanzo yasogezwa Wilaya ya Ubungo

CCCC Yaandaa Tamasha La Dragon Boat

Dkt. Biteko ashiriki kilele cha miaka 60 JWTZ

JOWUTA Yataka Sheria Za Kazi Kuwalinda Wafanyakazi Katika Vyombo Vya Habari

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Tume  Ya Ulinzi  Wa Taarifa Binafsi Yaongeza Muda Wa Taasisi Kujisajili
Next Article Kiwanda cha Sukari Mkulazi Chaanza Kuleta Tija, Sangu Apongeza Uwekezaji wa NSSF na Magereza
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?