MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mkurugenzi Mkuu Wa NSSF Aongoza Utoaji Wa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii Soko La Tegeta Nyuki
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mkurugenzi Mkuu Wa NSSF Aongoza Utoaji Wa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii Soko La Tegeta Nyuki
Habari

Mkurugenzi Mkuu Wa NSSF Aongoza Utoaji Wa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii Soko La Tegeta Nyuki

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, amesema hakuna sababu kwa mwananchi aliyejiajiri kushindwa kujiunga na Mfuko huo, kutokana na maboresho makubwa yaliyofanyika ambayo yanawawezesha wanachama wa kundi hilo kunufaika na mafao mbalimbali sawa na waajiriwa wa sekta ya umma na binafsi.
Mshomba ametoa kauli hiyo wakati alipowaongoza wafanyakazi wa NSSF kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na kuandikisha wanachama wapya katika soko la Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, kupitia kampeni ya NSSF Staa wa Mchezo Paka Rangi.
Amesema mwananchi aliyejiajiri atakapojiunga na NSSF atanufaika na mafao mbalimbali yakiwemo pensheni ya uzeeni, urithi, ulemavu, uzazi, matibabu pamoja na mafao mengine ambayo awali hayakupatikana kwa kundi hilo.
“Tunaposema wanachama wa NSSF ni mastaa wa mchezo, tunamaanisha kuwa Mfuko unatoa uhakika wa maisha bora, huduma za matibabu na kipato hata baada ya mwanachama kustaafu.
Habari Picha 10852
“Endapo mwanachama atafariki, wategemezi wake watanufaika na mafao ya urithi,” amesema.
Aliongeza kuwa NSSF imeboresha mfumo wa uchangiaji kwa kuufanya kuwa rahisi na rafiki kwa wananchi.
Amefafanua kuwa mwananchi anayechangia Sh. 30,000 kwa mwezi atanufaika na mafao yote ikiwemo matibabu, huku anayechangia Sh. 52,200 kwa mwezi atanufaika yeye, mwenza wake pamoja na wategemezi wasiozidi wanne.
Mshomba ameeleza kuwa uchangiaji si lazima ufanyike kwa mkupuo mmoja, bali unaweza kufanyika kwa utaratibu wa kila siku, wiki, mwezi au msimu, kupitia mifumo ya malipo ya kidijitali bila ulazima wa mwananchi kufika ofisi za NSSF.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Omary Mziya, amewahamasisha wananchi waliojiajiri kujiunga na kuchangia kwa ajili ya maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Naye Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, Lulu Mengele, amesema kampeni ya NSSF Staa wa Mchezo Paka Rangi itaendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa soko hilo, Katibu wa Soko la Tegeta Nyuki, Omary Hemed, ameishukuru NSSF kwa kuendelea kuwafikia wananchi sokoni hapo kwa kutoa elimu ya hifadhi ya jamii na kuwapa fursa ya kujiunga na kuchangia, hatua ambayo imewawezesha wengi kunufaika na mafao mbalimbali yakiwemo ya matibabu.
Habari Picha 10853
  • Habari Picha 10854
    Habari Picha 10855
    Habari Picha 10856
    Habari Picha 10857
    Habari Picha 10858
    Habari Picha 10859
    Habari Picha 10860
    Habari Picha 10861
    Habari Picha 10862
    Habari Picha 10863
    Habari Picha 10864
    Habari Picha 10865
    Habari Picha 10866
    Habari Picha 10867
    Habari Picha 10868
    Habari Picha 10869
    Habari Picha 10870
    Habari Picha 10871
    Habari Picha 10872
    Habari Picha 10873
    Habari Picha 10874
    Habari Picha 10875
    Habari Picha 10876

You Might Also Like

Sababu Nne Zilizofanikisha Mafanikio Katika Uandikishaji

Majaliwa Aituza UDSM kwa Kuongoza Eneo La Elimu, Utafiti, Ubunifu Sabasaba 2025

Tunatekeleza Azma YA Rais Samia Kuwafikia Wananchi Waliojiajiri

Tanzania Na Namibia Kuongeza Juhudi Kukuza Ushirikiano Wa Kiuchumi

Zungu Achaguliwa Kuwa Spika Mpya Wa Bunge La 13

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article DIB: Wenye Amana Benki Zilizofungwa Kulipwa Ndani ya Mwezi Mmoja
Next Article Luswetula Aagiza Udhibiti Mkali wa Mikopo Kandamizi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Mbunge Asisitiza Sheria za Majiko Safi Ili Kulinda Mazingira
Habari February 3, 2026
Mwalunenge: Bila Rasilimali Watu Na Mtaji, Mipango Ya Kilimo Haitafanikiwa
Habari February 3, 2026
Gulamali Ahoji Bungeni Changamoto ya Mawasiliano Ilongelo
Makala February 3, 2026
Serikali Yaendelea Kuimarisha Uhuru wa Mahakama – Nchimbi
Habari February 2, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?