MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Katambi Aagiza Ushindani Wa Haki Ili Kulinda Bei, Walaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Katambi Aagiza Ushindani Wa Haki Ili Kulinda Bei, Walaji
Habari

Katambi Aagiza Ushindani Wa Haki Ili Kulinda Bei, Walaji

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara, Patrobas Katambi, amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na Baraza la Ushindani (FCT) kuhakikisha ushindani wa haki katika biashara, hususan kuondoa ukiritimba na kupandishwa kwa bei za bidhaa na huduma.
Akizungumza katika ziara yake Baraza la Ushindani, Katambi amesema ushindani wa haki ni msingi wa ukuaji wa biashara, huku akibainisha kuwa biashara zinapaswa kulinda maslahi ya walaji, kuhakikisha bidhaa zenye ubora, na kufuata sheria kwa haki.
Ameongeza kuwa maboresho ya mgawanyo wa kazi kati ya Tume ya Ushindani na Baraza yamepunguza mzigo na kuongeza ufanisi, huku utulivu ukiwa umeimarishwa katika mazingira ya biashara.
Habari Picha 10690
Katambi amesisitiza Serikali inaendelea kuhamasisha uwekezaji kwa sera rafiki na maboresho ya kisheria, huku utatuzi wa migogoro ukipewa kipaumbele ili kulinda heshima, muda na maslahi ya wawekezaji.
Aidha, amesema usimamizi wa sheria za ushindani unalenga kumlinda mlaji na kuhakikisha ubora wa huduma, huku utatuzi wa migogoro kwa wataalamu wabobezi ukiimarisha imani katika sekta ya biashara.
Kwa niaba ya Jaji Rose Ibrahim, Dkt. Onesmo Kyauke amesema Baraza la Ushindani lina nafasi ya kipekee kuhakikisha sera za ushindani zinatekelezwa, kuvutia uwekezaji na kulinda maslahi ya walaji.
Ameongeza kuwa Tanzania iko katika kipindi cha ukuaji wa biashara na viwanda, huku Baraza likijipanga kuwa la kisasa na lenye weledi wa hali ya juu kushughulikia changamoto za soko kwa haki na haraka.
Habari Picha 10691

You Might Also Like

Tanzania Yatumia Wiki Ya Nishari India Kunadi Vitalu Vya Mafuta Na Gesi Asilia

Waajiri Wasilisheni Michango Kwa Wakati

UDSM Yamtunuku Rais AfDB Shahada Ya Heshima Ya Sayansi

Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo 2030

Salum Mwalim: Hakuna Mtu, Taasisi Inayoweza Kuzuia Uchaguzi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Katambi Aitaka TIRDO Kuongoza Mapinduzi ya Kufufua Viwanda Nchini
Next Article Serikali Yasema Migogoro Ya Ndoa lliyotatuliwa Imeongezeka
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?