MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Petroli Yaendelea Kushuka Bei Desemba
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Petroli Yaendelea Kushuka Bei Desemba
Habari

Petroli Yaendelea Kushuka Bei Desemba

Author
By Author
Share
2 Min Read

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa  za mafuta aina ya petroli zitakazotumika hapa nchini kwa  Desemba 2025, zikionesha kuendelea kushuka kwa bei ya petroli.

 

Ahueni hiyo inatokana  na kupungua kwa gharama za kuagiza mafuta katika bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa asilimia  2.4 kwa petroli, na asilimia 3.6 kwa mafuta ya taa.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule, leo, imebainisha kuwa, bei ya rejareja ya petroli imepungua kwa sh 2.38 (Dar es Salaam), 2.26 (Tanga) na sh 2.45 kwa Mtwara.

Aidha, bei ya mafuta ya taa kwa Dar es Salaam imepungua kwa sh 120.48 ikilinganishwa na bei za mwezi Novemba 2025.

 

Hivyo basi, bei za reja reja za petroli kwa mwezi huu, zitakuwa sh 2610.10, 2616.13 na 2616.24 kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia. Kwa upande wa dizeli, Dar es Salaam ni sh 2639.54, Tanga 2648.86 na Mtwara 2654.32.

 

Bei ya mafuta ya taa kwa Dar es Salaam ni sh 2513.87 huku bei za Tanga na Mtwara zikiwa hazina mabadiliko kutoka mwezi uliopita.

 

EWURA inawahimiza wauzaji wa mafuta nchini kutoa stakabadhi za mauzo kwa wanunuzi zinazoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita, kwani  stakabadhi hizo hutumika kama kithibiti kunapokuwa na changamoto yoyote kuhusu huduma hiyo.

 

Aidha, EWURA inavikumbusha vituo vyote vya mafuta nchini kuchapisha bei za bidhaa za mafuta  katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei, punguzo na vivutio vya kibiashara. Ni kosa kisheria kutoweka bango linaloonekana katika eneo la kituo na adhabu kali itatolewa kwa mujibu wa sheria kwa atakayekiuka.

You Might Also Like

JMAT Yatoa Neno Yanayoendelea Kwa Vijana Wa Kenya

VETA Shinyanga Yatumia Kompyuta Kubuni Bidhaa 

USAID yatoa Dola mil nane Kwa kampuni za Tanzania

Kamati Ya Bunge Ustawi Na Maendeleo Ya Jamii Yaridhishwa Wananchi Wanavyofikiwa

Serikali Yaja Na Kanuni Mpya Ya Sheria Ya Fidia   Kuboresha Mazingira Ya Mfanyakazi 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kikwete Awahimiza Wahitimu wa UDSM Kuwa Mabalozi Wazuri wa Chuo 
Next Article Mpango Wa Taifa Wa Teknolojia Uko Mbioni Kuja-Serikali
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Msama Aipongeza Hotuba Ya Samia, Atoa Neno Kwa Vijana, Wazee, Wanaharakati
Habari December 4, 2025
Profesa Silayo Aaga, Jawara Kuchukua Uongozi Mpya wa AFWC25
Habari December 3, 2025
Mpango Wa Taifa Wa Teknolojia Uko Mbioni Kuja-Serikali
Habari December 3, 2025
Kikwete Awahimiza Wahitimu wa UDSM Kuwa Mabalozi Wazuri wa Chuo 
Uncategorized December 2, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?