MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Palamagamba Kabudi, amepongeza ubunifu wa kutoa vitabu kwa njia ya sauti, akisema teknolojia hiyo itawasaidia watu wasiopata muda wa kusoma vitabu.
Waziri Kabudi alitoa pongezi hizo alipotembelea banda la Kampuni ya Uchapishaji Vitabu ya Mkuki na Nyota katika Maonesho ya 32 ya Kitaifa ya Vitabu Tanzania yanayoendelea Dar es Salaam.
Habari Picha 10408
Amesema wazo la vitabu vya sauti ni muhimu kwa kuwa msomaji anaweza kusikiliza popote alipo, Aidha, amesisitiza kuwa  kwa kuanza na vitabu vya Shaaban Robert kutawavutia vijana wengi.
“Kwa kuanza na aina hii ya vitabu tunawarithisha watoto wetu utajiri mkubwa wa maarifa. Naamini Maktaba ya Taifa nayo itafikiria kuwa na vitabu vya sauti, jambo litakalowasaidia hata watu wenye uoni hafifu,” amesema.
Habari Picha 10418
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchapishaji ya Mkuki na Nyota, Mkuki Bgoya, amesema kampuni hiyo inatengeneza vitabu vya sauti kwa kuvisoma na kuvipatia ladha kulingana na mahitaji ya kila kitabu.
Ameeleza kuwa wana platform ya mtandaoni iitwayo Digidigi Digital ambayo inawawezesha watu kusikiliza vitabu wakiwa katika mazingira mbalimbali kama vile wakiendesha gari au wakiwa nyumbani.
Pia, teknolojia hiyo inawanufaisha watu wasioweza kuona.
Bgoya amesema wameshaanza kurekodi mfululizo wa vitabu vya Shaaban Robert, vitabu vya viongozi, na vitabu vya watoto kama Hadithi za Katope.
Pia wameandaa vitabu vya sauti vya wasifu wa watu maarufu, na kazi hiyo inaendelea.
Hadi sasa, kampuni hiyo imerekodi vitabu 50 vya sauti, na inapanga kuwa na app maalumu ambayo watumiaji watalipia ada ya mwezi ili kusikiliza maudhui yote. Vitabu hivyo vimetayarishwa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
Aidha, wanatarajia kuwa na master classes, ambapo wataalumu mbalimbali watatoa mafunzo kuhusu mada tofauti kupitia mfumo huo.
Bgoya amesema teknolojia hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Januari 2026.

You Might Also Like

Roman Glorig Ahuisha Mkataba wa Uwakilishi wa Heshima wa Tanzania Nchini Czech

Ridhiwani Kikwete Azindua Miradi Ya Thamani Ya Bil. 1.7 Songwe

VETA Yafanya Mageuzi Makubwa Yaliyowezesha Wengi Kuajiriwa

TARI Yawaalika Wakulima Kujifunza Teknolojia Bora 88 Mkoani Morogoro

Idadi Ya Wagonjwa Wa Magonjwa Yasiyoambukiza Kuongezeka

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
Viongozi Wa Dini Zote Wajifungie Kuomba,Kujadili Na Kutoa Mapendekezo-SAU
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?