MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Mbunge Ndoinyo Kubadilisha Taswira ya Ngorongoro Na Kuimarisha Utalii, Ufugaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Mbunge Ndoinyo Kubadilisha Taswira ya Ngorongoro Na Kuimarisha Utalii, Ufugaji
Habari

Mbunge Ndoinyo Kubadilisha Taswira ya Ngorongoro Na Kuimarisha Utalii, Ufugaji

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Ngorongoro, Yanick Ndoinyo, amesema jimbo hilo ni la kimkakati kwa kuwa ni eneo maarufu kwa utalii, ufugaji na kilimo, hivyo anatambua kuwa ana majukumu mazito ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Akizungumza na wanahabari katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Ndoinyo amesema amejipanga kuhakikisha changamoto zilizopo wilayani zinabadilishwa kuwa fursa za maendeleo.
Amesema Kipaumbele chake cha awali ni kubadilisha taswira ya wilaya na kuimarisha mahusiano mazuri kati ya serikali na wananchi, ili mipango ya maendeleo ipokelewe kwa urahisi na kwa maelewano makubwa.
Ameeleza kuwa, kwa bahati mbaya, wilaya ya Ngorongoro ipo pembezoni na makao makuu yake bado yanaonekana ya kijijini,lengo ni kujenga barabara ya lami inayounganisha wilaya hiyo na mkoa wa Arusha, pamoja na kuifanya  kuwa kivutio kikubwa cha utalii.
Kwa sasa, fursa za utalii zinatekelezwa kwa takribani asilimia 50, hivyo dhamira ni kuzitekeleza kwa asilimia 100.
Aidha, amesema sekta ya ufugaji inapaswa kubadilishwa na kuendeshwa kibiashara zaidi, badala ya kutegemea mila kama ilivyo sasa.
Pia, ni ndoto yake kuhakikisha wilaya inapata mfuko wa kutunisha mitaji utakaowawezesha wananchi kujiajiri na kuongeza kipato chao.
Ndoinyo amesisitiza kuwa mikakati yote hiyo itafanikiwa endapo kutakuwepo na ushirikiano mzuri kati ya wananchi na serikali yao. Lengo kuu ni kuhakikisha serikali, wilaya, wananchi na taifa wanazungumza lugha moja kuhusu maendeleo ya Ngorongoro.
Ameongeza kuwa ni muhimu Watanzania waendelee kuwa na imani na Bunge la 13, ambalo linafahamu changamoto za wananchi na lina wabunge wengi wa CCM wanaotekeleza Ilani ya chama kwa ufanisi.
Katika awamu yake ya kwanza, Ndoinyo amesema atatumia mahusiano na uzoefu wake wa kimataifa kutekeleza miradi mbalimbali, kuboresha taswira ya Bunge kwa wananchi, na kuongeza imani yao kwa chombo hicho cha uwakilishi.

You Might Also Like

Kamati Ya Bunge Yahimiza Maslahi Ya Watumishi Wapya Yazingatiwe

Bodi Ya Wadhamini Ya NSSF Yaridhishwa Na Uwekezaji Wa Ubia Na Jeshi La Magereza

VETA yawafikia madereva ‘Boda boda’

Tanesco yashauriiwa kuendeleza kasi

TARI Yakutanisha Wadau Afya Ya Udongo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kadogosa: Serikali Yatenda Haki Kwa Wakulima, Wafugaji, Wananchi Wa Vijijini
Next Article Kagae: Waziri Mkuu Ajaye Atamsaidia Rais Samia Kuongeza Kasi ya Maendeleo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?