MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Kadogosa: Serikali Yatenda Haki Kwa Wakulima, Wafugaji, Wananchi Wa Vijijini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Kadogosa: Serikali Yatenda Haki Kwa Wakulima, Wafugaji, Wananchi Wa Vijijini
Habari

Kadogosa: Serikali Yatenda Haki Kwa Wakulima, Wafugaji, Wananchi Wa Vijijini

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE wa Bariadi Vijijini, Masanja Kadogosa, ameipongeza Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayowanufaisha wakulima, wafugaji na wananchi wa vijijini.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma, Kadogosa amesema sekta ya kilimo imepiga hatua kubwa kupitia ruzuku za mbolea na pembejeo, pamoja na programu mbalimbali za kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji.
“Ruzuku hizi zimeleta unafuu mkubwa kwa wakulima wetu. Kwa upande wa wafugaji, serikali imeendelea kutoa chanjo za mifugo na kujenga majosho katika maeneo mbalimbali. Katika ilani mpya ya CCM, tumewekewa mpango wa kuongeza maeneo ya malisho kutoka ekari milioni tatu hadi milioni sita ,” amesema Kadogosa.
Mbunge huyo ameongeza kuwa, licha ya mafanikio hayo, bado suala la maji vijijini limepewa kipaumbele maalum.
“Kwa sasa, upatikanaji wa maji vijijini ni asilimia 80.9, lakini bado mahitaji yetu ni makubwa. Tuna mradi mkubwa wa Shilingi Bilioni 440 unaotekelezwa sasa, ambao utapita Busega, Bariadi Mjini, Bariadi Vijijini, Kitilima na Meatu. Mradi huo ukikamilika, tutaondokana kabisa na changamoto ya maji,” amesema.
Kadogosa pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza Spika mpya wa Bunge, Mussa Zungu, akisema ana imani ataendesha Bunge lenye ushirikiano na Serikali kwa kuzingatia misingi ya kikatiba.
“Tunatarajia kuwa na bunge lenye mijadala yenye tija kwa wananchi. Spika Zungu ana uzoefu mkubwa, na naamini ataongoza Bunge letu kwa hekima, kuhakikisha bajeti na sheria zinazopitishwa zinaakisi mahitaji halisi ya Watanzania,” amesema.
Kadogosa amesema kuwa mafanikio haya yanaonyesha utekelezaji thabiti wa ilani ya CCM na dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wa vijijini wanapata huduma bora na maendeleo endelevu.

You Might Also Like

Tanzania Kuweka Muongozo wa Kitaifa wa Usimamizi wa Takwimu Kidijitali

SEforALL Kuimarisha Ushirikiano Upatikanaji Nishati Endelevu

VETA kushirikiana na Toyota Tanzania kuboresha mafunzo ya ufundi magari

Silaa: Akili Mnemba, Roboti kuongeza ufanisi,ubunifu 

Wahandisi 428 Wajengewa Uwezo Kukuza Taaluma

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Spika Mussa Zungu Atoa Hotuba Baada Ya Kuchaguliwa
Next Article Mbunge Ndoinyo Kubadilisha Taswira ya Ngorongoro Na Kuimarisha Utalii, Ufugaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tume Ya Ulinzi Wa Taarifa Binafsi Yatoa Siku Saba Kwa Taasisi Kujisajili
Habari June 12, 2026
Teknolojia Ya Juisi YA Ndizi Kali Yafungua Fursa Mpya Za Viwanda, Ajira
Makala Uncategorized June 12, 2026
Serikali Yaingia Makubaliano Ya Ushirikiano Na DIT Kuimarisha Usimamizi Wa Mataifa
Habari June 8, 2026
Wananchi Waelimishwa Masharti ya Kubadilisha Noti Zilizochakaa, Kuungua na Kuchanika
Habari June 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?