MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Chatanda Ampongeza Samia, Aahidi Kuinua Wanawake Kiuchumi
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Chatanda Ampongeza Samia, Aahidi Kuinua Wanawake Kiuchumi
Habari

Chatanda Ampongeza Samia, Aahidi Kuinua Wanawake Kiuchumi

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Lucy Ngowi
DODOMA: MBUNGE mteule wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa ushindi mkubwa wa kura asilimia 97.6, akisema matokeo hayo yanaashiria imani kubwa ambayo Watanzania wanayo kwake kutokana na kazi kubwa alizozifanya katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Chatanda amesema UWT, kwa niaba ya wanawake wote nchini, inampongeza Rais Samia kwa mafanikio hayo na inaahidi kushirikiana naye katika kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030, ili kuhakikisha ahadi zote zilizotolewa kwa wananchi, hasa wanawake, zinatimia.
Habari Picha 10241
“Kama mbunge mteule wa viti maalum, nipo tayari kuisimamia utekelezaji wa ilani ya chama chetu. Tutahakikisha tunafuatilia utekelezaji wake ili wananchi, hususan wanawake, wanufaike na maendeleo yaliyopangwa,” amesema Chatanda.
Ameongeza kuwa UWT itakuwa karibu na wanawake katika ngazi zote, kusikiliza kero na changamoto zao, zikiwemo ukatili wa kijinsia na changamoto za kiuchumi, ili hatua madhubuti zichukuliwe kupitia Bunge na Serikali.
Kuhusu uwezeshaji wa wanawake, Chatanda amesisitiza kuwa Rais ameonyesha dhamira ya dhati ya kuinua uchumi wa wananchi kwa kutenga Sh. Bilioni 200 ndani ya siku 100 za kwanza za uongozi wake, kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo, wakiwemo wanawake.
“Tutahakikisha wanawake wanapata mikopo ya asilimia 10 kutoka halmashauri zetu na kwamba fedha hizo zinatumika ipasavyo. Hatuishii kutoa mikopo tu; tutahakikisha akinamama wanapewa elimu na mafunzo ya matumizi bora ya fedha hizo, ili ziweze kuwanufaisha na kuwainua kiuchumi,” amesema.
Chatanda amesisitiza kuwa jukumu kubwa la UWT ni kuhakikisha kila mwanamke anapata fursa ya kujikomboa kiuchumi kupitia elimu, uwezeshaji na ufuatiliaji wa sera za maendeleo zinazogusa maisha yao.

You Might Also Like

Ridhiwani, Mlao na wanachama wa CCM Kata ya Bwilingu wakinadi chama chao dakika za lala salama

Vijana 26 Kwenda Kujifunza Mafunzo Ya Vitendo Nje Ya Nchi

Kamati Ya Bunge Yahimiza Maslahi Ya Watumishi Wapya Yazingatiwe

Bajeti ya TUGHE 2025 Yaidhinishwa

Ridhiwani Ateta na Viongozi wa Vijiji Lugoba, Chalinze 

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Watumishi Wa Afya Waliofadhiliwa Watakiwa Kukamilisha Taratibu Ifikapo Novemba 22,2025
Next Article Rita Kabati Aahidi Kuimarisha Miundombinu, Kuwatumikia Wananchi Wa Kilolo
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?