MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watumishi Wa Afya Waliofadhiliwa Watakiwa Kukamilisha Taratibu Ifikapo Novemba 22,2025
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watumishi Wa Afya Waliofadhiliwa Watakiwa Kukamilisha Taratibu Ifikapo Novemba 22,2025
Habari

Watumishi Wa Afya Waliofadhiliwa Watakiwa Kukamilisha Taratibu Ifikapo Novemba 22,2025

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Lucy Lyatuu

WIZARA ya Afya imesema kwa mwaka wa fedha 2025/26,  imetenga jumla ya Sh bilioni 13.6 ukilinganisha Sh bilioni 10.95 zilizotengwa mwaka wa fedha 2023/24 hivyo kufanya ongezeko la Sh bilioni 2.73 sawa na asilimia 25.

Kwa mujibu wa taarifa ya  Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Roida  Andusamile azma ya Serikali ni kuongeza bajeti ya mafunzo ya wataalam bingwa na bobezi katika fani mbalimbali za Sekta ya afya kila inapowezekana.

Amesema  Wizara ya Afya inawahimiza watumishi wote waliopata ufadhili kwa mwaka 2025/26 kukamilisha taratibu za kujaza mikataba ya ufadhili kama ishara ya kukubali ufadhili huu kabla au ifikapo  Novemba 22, 2025.

Amesema katika mwaka wa fedha 2025/26 maombi ya ufadhili 1,074 yaliwasilishwa na kati ya hayo, waombaji 981 walikidhi vigezo vya kufadhiliwa na waliochaguliwa kwa ajili ya ufadhili kulingana na fedha iliyotengwa ni 498 sawa na asilimia  51 ya waombaji waliokidhi vigezo.

Amesema fedha iliyotengwa itatumika kufadhili watumishi wapya 498 pamoja na 985 wanaoendelea na masomo katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi na kufanya jumla ya watakaofadhiliwa kwa mwaka 2025/26 kuwa 1,483.

Aidha, kati ya watumishi 498 waliochaguliwa kupata ufadhili, watumishi 442  wamechaguliwa kupata ufadhili katika vyuo vikuu vya ndani ya nchi na 56  wamepata ufadhili katika vyuo vya nje ya nchi kwakuwa taaluma wanaozoenda kusoma hazipatikani katika vyuo vya ndani ya nchi.

Amesema Wizara imezingatia vipaumbele muhimu vya kisekta kama ubobezi katika ngazi mbalimbali za huduma Pamoja  na vipaumbele kama vilivyoainishwa kwenye Mpango Mkakati wa Tano wa Sekta ya Afya pamoja na bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/26.

 

Amevitaja vipaumbele hivyo ni Pamoja na taaluma za kuimarisha huduma za watoto, uzazi na magonjwa ya wanawake, saratani, magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama ya moyo na figo, matibabu ya ubongo na mishipa ya fahamu, afya ya akili, afya ya kinywa na meno, huduma mahsusi za upasuaji ikiwemo masikio, pua na koo, huduma za utengemao na tiba shufaa, ugunduzi wa magonjwa ikiwemo patholojia.

Amesema nakala ya mkataba inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya afya na pia itatumwa kupitia anuani za barua pepe walizotumia wakati wa kuwasilisha maombi.

Nakala tatu (halisi) za mkataba zilizojazwa pamoja na barua za wadhamini ziwasilishwe katika ofisi ya Wizara ya Afya Makao Makuu, Mtumba Jijini Dodoma.

 

“ Ufadhili huu ni kwa ajili ya kulipiwa ada ya mafunzo na posho ya utafiti kwa watakaofadhiliwa ndani ya nchi,” amesema na kuongeza kuwa kwa wale watakaosoma vyuo vya nje ya nchi watalipiwa ada, posho ya kujikimu wakiwa masomoni, nauli ya kwenda na kurudi pamoja na posho ya utafiti.

Aidha amesema malipo ya posho ya utafiti na posho ya kujikimu yatazingatia viwango vilivyopangwa na Wizara.

 

 

You Might Also Like

Soko La Kisasa La Nyamachoma Lazinduliwa Vingunguti

Aloe Dorotheae, Mmea Unaopatikana Tanzania Pekee

Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, Laleta Furaha Kwa Watoto

Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu yaita wawekezaji

Majaliwa Akazia Disemba Ni Mwisho wa Kutumia Mkaa. Gesi Kweny Taasisi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Zungu Achaguliwa Kuwa Spika Mpya Wa Bunge La 13
Next Article Chatanda Ampongeza Samia, Aahidi Kuinua Wanawake Kiuchumi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Vitabu Vya Sauti Kuvutia Vijana, Serikali Yapongeza Ubunifu Wa Mkuki Na Nyota
Habari November 22, 2025
Ubora Wa E & D Vision Publishing Wamkuna Waziri Kabudi Maonyesho Ya Vitabu Dar
Habari November 22, 2025
Kabudi: Vitabu Ni Tiba, Atoa Wito Kuimarisha Maktaba, Uchapaji 
Habari November 22, 2025
Kwagila Awataka Wasimamizi Wa Elimu TAMISEMI Kuwajibika Kikamilifu
Habari November 21, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?