MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wizara Ya Madini Kununua Chopa, Kufanya Utafiti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wizara Ya Madini Kununua Chopa, Kufanya Utafiti
Habari

Wizara Ya Madini Kununua Chopa, Kufanya Utafiti

Author
By Author
Share
2 Min Read
Na Danson Kaijage
DODOMA: WIZARA ya Madini imejipanga kununua chopa ambayo itafungwa mitambo kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina nchi nzima kwa lengo la kubaini kiwango cha madini yanayopatikana na aina yake.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini Anthony Mavunde alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara hiyo kwa Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo Jijini Dodoma.
Mavunde amesema chopa itakayonunuliwa na kufungwa mitambo ya kufanya utafiti wa madini nchini itakuwa na uwezo wa kubaini kitu kilichopo chini ya ardhi kwa umbali wa mita 500.
Amesema kwa nchi ya Tanzania licha ya kuwa inafanya vizuri katika sekta ya madini lakini bado,  kwani ni asilimia 16 tu ya utafiti uliofanywa ambao unakubalika kimataifa.
“Tutakapokuwa na chopa ambayo itafungwa mitambo ya kisasa ya kufanya utafiti wa kubaini madini na aina yake tutaweza kufanya utafiti wa kina ambao unakubalika kimataifa.
“Kwa kutambua umuhimu wa sekta ya madini Rais Samia ameipatia sekta hiyo pesa nyingi,kwa mwaka wa fedha 2024/25 tulipatiwa bajeti ya Sh. Bilioni 231 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake na pesa nyingi imewekezwa kwenye utafiti.
“Kwa sasa utafiti kina uliofanywa nchi nzima ni asilimia 16 tu lakini mkakati uliopo ni ifikapo 2030 kutakuwepo na asilinia 50 ya upimaji wa kina nchi nzima na hapa sekta ya madini itakuwa na uhakika wa kutambua kiasi cha madini yanayopatikana nchini na aina zake,” amesema.
Amesema jambo lingine la mafanikio ni ujenzi wa maabara kubwa na ya kisasa itakayojengwa Dodoma eneo la kizota jambo ambalo ameeleza kuwa ni kuyaongezea madini thamani.
Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa madini yanalenga kumnufaisha mtanzania mzawa yakiwemo makundi ya vijana,wanawake na makundi maalum.

You Might Also Like

Rais Samia aweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa Suluhu Sports Academy

Nchimbi Agongelea Nyundo Kwa Wagombea Watoa Rushwa

UDSM Yatumia Teknolojia Ya Kidijitali Kukabili Sumukuvu

VETA Yatahadharisha Changamoto ya Kuzidisha Uchanganyaji wa Chakula Cha Mifugo

UDSM Yaanzisha Mkakati Kuokoa Nyuki Wadogo

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Serikali Kupeleka Umeme Maeneo Ya Kimkakati
Next Article Maziwa Kukuza Uchumi Wa Wafugaji
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?