MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waziri Sangu Aagiza Hatua Kali kwa Waajiri Wanaokwepa Kuwasilisha Michango NSSF
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waziri Sangu Aagiza Hatua Kali kwa Waajiri Wanaokwepa Kuwasilisha Michango NSSF
Habari

Waziri Sangu Aagiza Hatua Kali kwa Waajiri Wanaokwepa Kuwasilisha Michango NSSF

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
3 Min Read
Awataka kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati
Na Mwandishi Wetu
DODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu,  Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amewaagiza viongozi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)  kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya waajiri wa sekta binafsi wanaoshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati, akisisitiza kuwa kitendo hicho kinawanyima wafanyakazi haki zao za msingi ikiwemo mafao ya uzeeni.
Sangu ametoa maelekezo hayo Desemba 17, 2025 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Ofisi za NSSF jijini Dodoma, ikiwa ni ziara yake ya kwanza  tangu alipoteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Habari Picha 10571
Katika ziara hiyo, aliambatana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Mahusiano, Rahma Kisuo.
Amesema  ni wajibu wa kisheria kwa kila mwajiri wa sekta binafsi kujiandikisha katika Mfuko, kuwaandikisha wafanyakazi wake na kuwasilisha michango yao kwa wakati kila mwezi.
Waziri huyo amesisitiza kuwa Serikali haitavumilia uzembe au makusudi ya kukiuka sheria kwa waajiri wanaohatarisha mustakabali wa wafanyakazi wao.
“Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, hakikisha waajiri wote wasiowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati wanachukuliwa hatua za kisheria bila muhali, kwani wanaposababisha kucheleweshwa kwa mafao, huwaumiza wafanyakazi waliolitumikia taifa kwa muda mrefu,” amesema Sangu.
Aidha, Waziri huyo ameipongeza NSSF kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita, akitaja ongezeko la wanachama na waajiri, kuimarika kwa makusanyo ya michango, mapato ya uwekezaji, kuongezeka kwa thamani ya Mfuko pamoja na maboresho ya malipo ya mafao kwa wanachama.
Habari Picha 10572
Akitoa taarifa ya utendaji wa Mfuko, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,  Masha Mshomba, amesema katika kipindi cha miaka mitano kinachoishia Juni 30, 2025, Mfuko umeongeza idadi ya wanachama wapya kutoka 215,693 mwaka 2020/21 hadi 363,925 mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 68.72.
Ameongeza kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/26, Mfuko uliandikisha wanachama wapya 111,881, sawa na asilimia 110 ya lengo, huku kwa mwaka mzima wa fedha 2025/26 ukitarajiwa kuandikisha wanachama wapya 447,523, wakiwemo 316,957 kutoka sekta rasmi na 130,566 kutoka kwa wananchi waliojiajiri.
Mshomba amesema hadi kufikia 30 Septemba 2025, idadi ya wanachama wachangiaji imeongezeka na kufikia 1,703,821 ikilinganishwa na 932,112 waliokuwepo Juni 2021, sawa na ongezeko la asilimia 82.79, huku makusanyo ya michango yakiongezeka kutoka Sh. Blioni 1,171.97 hadi Bilioni 2,718.87, na thamani ya Mfuko kufikia Sh. trilioni 10.
Habari Picha 10573
Habari Picha 10574
Habari Picha 10575
Habari Picha 10576
Habari Picha 10577
Habari Picha 10578

You Might Also Like

VETA Kujenga Mahusiano Na Wenye Ujuzi, Wabunifu

Ridhiwani Aipongeza Mahakama Kuzingatia Ajira Kwa Wenye Ulemavu

HATUNA HURUMA NA WADANGANYIFU KWENYE MITIHANI – WAZIRI MKENDA

Samia Aleta Mapinduzi Arusha

BUWSSA Yapewa Bilioni 28 Kutatua Tatizo La Maji

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Maofisa Habari Wa Serikali Jipangeni  Kiteknolojia- Katibu Mkuu Kiongozi
Next Article Katambi Aitaka NDC Kuleta Mapinduzi Makubwa Ya Viwanda
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

CAG Aipongeza TARURA Kwa Ujenzi Wa Miundombinu
Habari January 9, 2026
Tuna Deni La Kusimamia Miradi Na Kusikiliza Kero za wananchi Ili Kuleta Maendeleo Ya Kweli-Salome
Habari January 9, 2026
Rais Dkt Samia Azindua Majengo Ya Kisasa
Habari January 8, 2026
TEA, UNICEF Watekeleza Miradi ya Elimu Visawani Zanzibar
Habari January 8, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?