Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo amewataka watumishi wa serikali kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji badala yake wawe msaada kwa wawekezaji kufikia malengo yao.
Ili kuwezesha uwekezaji kusonga mbele kwa kila mwenye jukumu kuhakikisha amelitimiza.
Ametoa rai hiyo alipotembelea kiwanda cha Lodhia kinachotengeneza mabati kilichopo Kisanvule , Mkuranga Kukagua shughuli zinazofanywa kiwandani hapo.
“Naomba uwekaji wa transfoma uwe umekamilika ndani ya wiki tatu ili kuhakikisha dhamira ya Rais Samia ya kuwa na viwanda inakamilika,” amesema.
Amesema kiwanda hicho kimetumia zaidi ya Shi bilioni 162 kufunga mitambo hivyo wanapaswa kuanza uzalishaji.
“Huo ni uwekezaji mkubwa ambao utaongeza ajira nchini na pato la taifa kwa ujumla. Uwekezaji umeendela kujipambanua na umeongeza wigo wa kupunguza tatizo la ajira.
“Nimeona baadhi ya changamoto ambayo serikali ikiweza kufanyia kazi viwanda hivi vitafanya uzallishaji na hiki kiwanda kipya kabisa kadhalika kitaanza uzalishaji,” amesema.
Kuhusu tatizo la trasfoma tayari Mamlaka ya Mapato Tanzania imeshakamilisha taratibu hivyo ni jukumu la Tanesco kulifanyia kazi ili umeme uwafikie wawekezaji wa Mkuranga.
Naye Mkurugenzi wa kiwanda cha Lodhia, Sailesh Pandit amesema kwa sasa kiwanda kimekamilika wanasubiri kupata umeme ili waanze uzalishaji.
Pandit amesema uzalishaji utakapoanza wanatarajia kuzalisha kati ya tani 5000 hadi 10000 kwa mwezi.
“Watanzania tunatakiwa kusaidiana na kuona fahari ya kununua bidhaa wanayoiona inavyotengezwa nchini kwao. Kuna kasumba fulani yakuona bidhaa za nje ni bora kuliko za ndani. Lakini niwahakikishie bidhaa zetu zinakidhi ubora wa kimataifa.
“ Baada ya wiki tatu tunaanza uzalishaji wa mabati kama ambavyo waziri amesema TRA wamekamilisha na kuruhusu transforma itolewe bandarini. Hapa tunasubiri Tanesco waje kufunga ili supply ya umeme iwepo,” said Pandit soko letu litaanza ndani na baadaye ukisha kuwepo utoshelevu tutakwenda Afrika Mashariki.
Amesema kwa sasa kiwanda kimetoa ajira ya moja kwa moja kwa watanzania 620,
pia kuna ajira ya isiyo ya moja kwa moja kama vibarua.
Naye mkuu wa Wilaya ya Mkuranga ,Hadija Ally amesema uwepo wa kiwanda hicho kitaongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja na wilaya pia.