MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Watanzania Acheni Kuchanganya Mazao -Jafo
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Watanzania Acheni Kuchanganya Mazao -Jafo
Habari

Watanzania Acheni Kuchanganya Mazao -Jafo

Author
By Author
Share
3 Min Read

Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo ametoa rai kwa Watanzania kuacha kuchanganya mazao ili kutokuharibu au kupunguza thamani ya mazao hayo katika soko la kimataifa na kuharibu taswira ya Tanzania.

Aidha ameliagizza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuendelea kusimamia na kufuatilia ubora wa Mazao hayo yanayohifadhiwa na kuuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani na Wakala wa Vipimo (WMA) kuhakikisha mizani zote nchini zinapima mazao kwa usahihi

Ameyasema hayo alipotembelea Ghala linalotumia Mfumo wa Stakabadhi ghalani wakati wa Ziara Maalum Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kuongea na Wananchi wa Maeneo hayo.

Ziara hiyo iliongozwa na Kauli Mbiu isemayo “Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone” iliyofanyika Mkoani humo.

Vilevile akiwa katika Ghala hilo amesema ameridhika na ujenzi wake na ameiagiza Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) ndani ya siku 20 kukaa kikao na Bodi ya Korosho ili kufanya tathimini ya siku ngapi zinafaa kutoa korosho gharani huku wakifanya utafiti wa kina kuhusu suala la unyaufu katika zao la Korosho ili kuhakikisha wananchi wanafaidika na mazao yao ya kilimo.

Aidha, katika ziara yake Wilayani humo amebainisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ujenzi shule za sekondari na zahanati imetumika vizuri na miradi hiyo imejengwa katika kiwango kinachohitajika na amewataka Watoto wa shule hizo kusoma kwa bidii ili wawe viongozi wa siku zijazo.

 

Waziri Jafo alikagua ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Kata
ya Kichonda, aliweka jiwe la msingi
kwenye ujenzi wa Zahanati
katika kijiji cha Ngorongopa, jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Bweni la
Watoto Maalum katika shule
ya Msingi Kambarage na alizindua jengo la vyumba 3 vya madarasa na matundu 3 ya vyoo katika shule ya
Msingi Luiza Mlelwa.

Akiongea na Wananchi wa liwale Dkt Jafo amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendele kutatua changamoto mbalimbali walizonazo ikiwemo kuweka mindominu wezesheshi ya barabara , maji na umeme ili luhakikisha uchumi wa nchi hii inaongea na kukuza uchuma

Naye Mkuu wa Wilaya ya Liwale Goodluck Mlinga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo.

Ameahidi Wilaya yake itaendelea kusimamia Miradi hiyo kikamilifu na kuwataka Wananchi wa Wilaya hiyo kutumia fursa za miradi hiyo ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Asangye Bangu amebaimisha kuwa atatekeleza maelekezo yaliyotolewa na kuwataka Wananchi kuendelea kutumia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani unaowawezesha wakulima kuuza mazao hayo kwa bei nzuri na kuwataka Wananchi hao kuweka ghalani mazao yenye ubora unaotakiwa.

You Might Also Like

Trilioni 1.3  Zatumika Kuboresha Afya Ya Msingi Nchini

WDC Kuboresha Miradi Yake Ya Majengo

Kagera, Geita kuanza uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura

Tanzania Ipo Tayari Soko la Pamoja kuuziana Umeme – Biteko

CCM Kuwezesha Wananchi Kufuatilia Mkutano Mkuu Maeneo Ya Wazi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Kameta awaasa watanzania kutonunuliwa  kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mtaa, Mkuu
Next Article Watanzania Tuendelee Kudumisha Amani-Dk Biteko
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

NSSF Yaendelea Kutoa Elimu Ya Hifadhi Ya Jamii ‘ Karibu Tukuhudumie’
Habari June 21, 2025
Wananchi Watakiwa Kutowachagua Watoa Rushwa
Habari June 19, 2025
Kihenzile: Mifumo Ijengwe Kuhakikisha Huduma Zinapatikana Kwa Haraka, Salama, Zenye tija
Habari June 19, 2025
MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani
Habari June 19, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?