MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti
Habari

Wataalamu wa Fedha SADC Wakutana Pretoria Kujadili Bajeti

Lucy Ngowi
By Lucy Ngowi
Share
2 Min Read
Na Mwandishi Wetu
WATAALAMU wa masuala ya fedha na bajeti kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamekutana jijini Pretoria, Afrika Kusini kujadili hali ya kifedha ya jumuiya hiyo pamoja na mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ya kikanda.
Kikao hicho cha Kamati ya Fedha cha SADC kinafanyika leo Machi 9, 2026 na kinahusisha wawakilishi wa nchi wanachama, akiwemo Kamishna wa Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha Tanzania, Rishade Bade, anayeongoza ujumbe wa wataalamu wa Tanzania.
Katika kikao hicho, wajumbe wanajadili hali ya michango ya nchi wanachama wa SADC pamoja na mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 kwa kipindi cha miezi tisa kuanzia Aprili hadi Desemba 2025.
Habari Picha 11381
Pia wanapitia mapendekezo ya bajeti ya jumuiya hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/27 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya SADC kwa kipindi cha muda wa kati kuanzia mwaka 2027/28 hadi 2030/31.
Aidha, wataalamu hao wanajadili kwa kina mikakati ya kuongeza rasilimali fedha  kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ya kikanda, pamoja na utekelezaji wa uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Kanda.
Habari Picha 11382
Taarifa zinaeleza kuwa nchi 11 kati ya 16 wanachama wa SADC, ikiwemo Tanzania, tayari zimesaini mkataba wa kuanzishwa kwa mfuko huo ambao unatarajiwa kuwa chanzo muhimu cha fedha kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo katika kanda hiyo.
Kikao cha Kamati ya Fedha ni miongoni mwa vikao vya maandalizi kuelekea Mkutano wa 47 wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika Machi 12 na 13, 2026.
Habari Picha 11382
Habari Picha 11386
Habari Picha 11385

You Might Also Like

Mchengerwa Apongeza Shule Ya Sekondari Kibaha Kwa Ufaulu Wa Hali Ya Juu

Kituo Cha Umahiri Cha Upandikizaji Figo, Mafunzo, Kujengwa Hospitali Ya Benjamin Mkapa

Waziri Mbarawa Aagiza Adhabu Kali kwa Madereva, Makondakta Wanaonyanyasa Wanafunzi

Rais Samia kufanya ziara mkoani Morogoro, kuzindua safari za SGR

Wananchi Uyui Wafurika Kumsubiri Mgombea Urais CCM

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article TASFAM Yawawezesha Wanawake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kuadhimisha Siku ya Mwanamke
Next Article Mtaka, Ndunguru Wakubaliana Ujenzi wa Maabara ya Kimkakati Njombe
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Nchimbi Ahimiza Ushirikiano wa Wizara Katika Uhifadhi wa Mazingira
Habari March 10, 2026
Mtaka, Ndunguru Wakubaliana Ujenzi wa Maabara ya Kimkakati Njombe
Habari March 10, 2026
TASFAM Yawawezesha Wanawake wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kuadhimisha Siku ya Mwanamke
Habari March 9, 2026
Nyamhokya Atoa Wito kwa Wanawake Kusimama Imara Kiuchumi
Habari March 7, 2026
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?