MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Wataalam wa “Visit Finland” Wabadilishana Uzoefu Kutangaza Utalii Duniani 
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Wataalam wa “Visit Finland” Wabadilishana Uzoefu Kutangaza Utalii Duniani 
Habari

Wataalam wa “Visit Finland” Wabadilishana Uzoefu Kutangaza Utalii Duniani 

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu,
KATIBU  Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amekutana na kubadilishana uzoefu wa mikakati ya kutangaza utalii na wataalamu mbalimbali wa utalii wa nchi ya Ufini (Finland).
Katika ziara yake inayoendelea nchini Ufini, Dkt. Abbasi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kuitangaza Tanzania, leo Oktoba 10, 2024, alianza kwa kukutana na Mjumbe wa “Team Finland” Kamati ya Kitaifa ya Sekta mbalimbali ya kuitangaza nchi hiyo, Balozi Paula Parviainen ambaye alieleza jinsi nchi hiyo inavyounganisha sekta mbalimbali katika jukumu moja la kitaifa la kuipa taswira njema nchi hiyo.
Baadaye alikutana na timu ya wataalamu wa “Business Finland” wanaosimamia pia Kikosi cha Kutangaza Utalii wa nchi hiyo kimataifa yaani “Visit Finland” wakiongozwa na Mkurugenzi Mwandamizi wa Masoko ya Kimataifa,  Heli Jimenez.
Jimenez  ametoa uzoefu wa namna Finland inavyotumia mandhari zake za misitu kuibua zao jipya la utalii uitwao “wellness.” huku Tanzania nayo ikitoa uzoefu wake hasa katika utalii wa safari za kuona wanyama.
Aidha  Katibu Mkuu na ujumbe wake amebadilishana uzoefu na mikakati na Timu ya wataalamu kutoka “Business Helsinki” wanaosimamia pia kampeni ya kiutalii ya jiji la Helsinki ya “Visit Helsinki” na kubadilishana uzoefu namna miji inavyoweza kutumia vivutio vyake kujitangaza kwa ajili ya utalii wa ndani na ule wa kimataifa.
Akitoa uzoefu wake, Meneja Mwandamizi wa Taarifa za Watalii na Ubunifu wa Maudhui, Mari Somero, amesema jiji la Helsinki pekee hupata hadi watalii milioni nne kwa mwaka na wameunda timu inayohakikisha kila sekta inatimiza wajibu wake katika kuufanya mji huo kuwa kivutio zaidi.
“Kila tulipokutana na wataalamu wenzetu hawa waliobobea zaidi katika kutangaza utalii mambo mawili yamejitokeza; mosi, wametumia sana mazingira yao kuibua mazao mchanganyiko ya utalii kama vile utalii wa misituni, wakati wa kiangazi na baridi na hata utalii wa mijini (urban tourism).
“Pili, wamewekeza bajeti kubwa kujitangaza kimataifa mpaka wana vituo maalum vyenye maafisa kamili wa utalii katika miji mikubwa ya Ulaya, Asia na Marekani na wametupa uzoefu pia jinsi walivyoshirikiana na kampuni kubwa inayosafirisha zaidi ya watalii milioni 400 kwenda sehemu mbalimbali ya Expedia ya Marekani,” amesema Dkt. Abbasi.
Finland ambayo, tofauti na Tanzania, bado haijarejea kwenye idadi yake ya kawaida ya watalii ikilinganishwa na kabla ya Uviko, kwa takwimu mwaka mmoja uliopita ina jumla ya watalii wa ndani na nje wapatao milioni 11 huku ikiwa na mapato ya Euro bilioni 3.4.

You Might Also Like

Takukuru Kinondoni Yapokea Malalamiko 46 Kuhusu Rushwa

TARI yapongezwa kwa kuwa na teknolojia bora za kilimo

Serikali Kukarabati Vituo Vyote Vya Kutolea Huduma Za Afya Kongwe

Mwanachama Wa TALGWU Akutwa Hana Hatia

VETA Yatafiti Dawa Ya UTI, Fangasi

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Rais Samia Awasili Mwanza Kilele Cha Mbio za Mwenge
Next Article CMA Inasaidia Vijana Kuwa Na Nafasi Bora Kazini
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Tulia Atoa Taarifa Kifo Cha Ndugai
Habari August 6, 2025
Tume ya Kurekebisha Sheria Yaelimisha Umma Kuhusu Haki za Wanyama
Habari August 6, 2025
Bundi Wasaidia Kupambana na Panya: Teknolojia Asilia Inayobadili Maisha ya Wakulima
Habari August 6, 2025
Ofisa wa TARI Kuwapo Kila Kituo cha Umwagiliaji – Naibu Katibu Mkuu
Habari August 6, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?