“Wengine walikwenda Ofisi za Kata, wengine kwa Mjumbe, wengine kwa Waziri, au kwa Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya lakini naomba ifahamike tu kwamba wafanyakazi wanatakiwa kutambua kwamba chombo ambacho kumeundwa rasmi kwa sheria ya Bunge ni Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kwa ajili ya kutatua migogoro ya kikazi.
“Kwa hiyo tunakumbushwa wafanyakazi kutambua kuwa unapopata mgogoro unatakiwa kwenda wapi na unatakiwa kuuwasilisha ndani ya muda gani kwa migogoro ya uachishwaji ni siku 30 na migogoro mingine yote ni ndani ya siku 60 kwa hiyo tuzingatie hilo ili tusikose haki zetu za msingi kwa sababu yoyote ile,” amesema.
Amesema iwapo mfanyakazi ana sababu za msingi za kuwasilisha maombi nje ya muda ni lazima ionekane katika macho ya sheria kama ni suala la ugonjwa mfano lazima kuwe na vyeti vya hospitali.
“Kuna wale ambao wanasema walikuwa wanatibiwa kienyeji, kutibiwa kienyeji hakuna ushahidi ambao utauwasilisha kuwa ulikuwa unatibiwa kienyeji, kwa hiyo ni vizuri kufuata taratibu ambazo zipo,
“Njia ambazo ni sahihi ambazo mwisho wa siku kwenye sheria itaonekana ulikuwa na sababu za msingi, nyaraka lazima ziwasilishwe na hizo nyaraka zionyeshe wazi kuwa hukuwa na uwezo wa kuwasilisha mgogoro wako kwa sababu za ugonjwa.
“Kwa sababu unaweza ukawa unaumwa lakini bado ukawa na uwezo wa kufanya shughuli zako nyingine huku unaendelea na matibabu, huo ugonjwa lazima uwe umekufanya ushindwe kuchukua hatua ya kufungua mgogoro wako,” amesema.
Ameongeza kuwa, wengine wanachangamoto ya kuwa mahabusu uwezekano wa kufungua mgogoro ni mdogo kwa sababu mgogoro wa kikazi lazima ufunguliwe na mfanyakazi husika tofauti na migogoro mingine ya madai ambayo wakili anaweza akafungua kwa niaba.
Amesema kwenye migogoro ya kikazi mfanyakazi ni lazima ajaze ile fomu namba moja ya kuwasilisha mgogoro mbele ya tume
“Kwa hiyo sababu ya kuwa mahabusu ni sababu ya msingi lakini mara utakapotoka unatakiwa kuchukua hatua sahihi za kuwasilisha mgogoro ndani ya wakati.
“Lakini sababu nyingine inayoweza kuwa ya msingi ni iwapo mfanyakazi labda alikuwa nje ya nchi kwa sababu ambazo ni za msingi na sio kwa sababu zake binafsi.
“Kwamba ameamua kwenda kufanya maisha yake mengine lakini iwe ni kwa sababu za msingi kwamba hakuweza kuwasilisha huo mgogoro mbele ya tume ndani ya wakati,”amesema.
Amesisitiza kuwa, CMA ni chombo pekee kinachoshughulika na utatuzi wa migogoro ya kikazi.