Na Lucy Lyatuu
SERIKALI inatarajia kuzindua dira itakayojenga uchumi utakaofikia dola takriban trilioni Moja katika miaka 25 ijayo.
Mkurugenzi Mtendaji Wa kituo Cha Ubia Kati ya sekta ya umma na binafsi(PPP) ,David Kafulila amesema hayo leo Dar ea Salaam wakati akizungumza kuanza kwa kongamano litakalojadili mwenendo Wa uchumi Kati ya sekta binafsi na ya umma kuelekea Tanzania ya 2050.
Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo hicho kwa kushirikiana na Taasisi Ya Mpango Wa Utafiti Na Elimu Ya Demokrasia Tanzania (REDET) chini ya uratibu Wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).
Amesema uchumi unaozungumziwa katika dira hiyo ni umeweza kufikiwa na nchi 19 peke yake ambapo ni muhimu kwa kuwa na kongamano hilo kwa ajili ya majadiliano zaidi.
Amesema kongamano hilo litafanyika kesho Jumanne Mei 27, 2025 katika Ukumbi wa Maktaba ya Chuo cha UDSM ambapo litakuwa ni kongamano la wazi watu lenye kushirikisha wanazuoni mbalimbali kutoa maoni .
Amesema kituo Cha Ubia kina jukumu la kushirikisha umma kuhisu masuala ya Ubia kwa lengo la kujenga uelewa unaofanana kuhusu kile ambacho serikali inafikiri na kile wananchi wanachofikiri.
Amesema hivyo Kituo kinawahibu Wa Kufanya umma uelewe masuala ya kisera,kisheria na mipango ya serikali kwenye maeneo hayo ya Ubia.
“Kwa kuona umuhimu ho ndioaana tumeshirikiana na REDET ili kushirikisha umma na wanazuoni kuwa sehemubya fikra ili kuona mfanano Kati ya serikali na sekta binafsi,” amesema Kafulila.
Amesema ni kongamano lenye kushirikisha wanazuoni na wataalam mbalimbali ili kuona mchango waoh kuelekea dira hiyo.
Kwa upande wake Mwenye kiti Wa REDET, Profesa Rwekaza Mkandala amesema mada kuu ni dola,masoko na uhamishaji Wa mitani.
Amesema katika mada hiyo itajadili nafasibya Ubia Kati ya sekta ya umma na binafsi kufikiwa malengo ya dira ya maendeleo ya Tanzania 2050.
Amesema wanatoka kuongeza ufahamu kuhusu sekta hizo na washiriki ni pamoja na wanazuoni,vyama vya siasa,Taasisi mbalimbali ili kudadavua na kuona kiwango cha uelewa .
Amesema mada mbalimbali zitatolewa ikiwa ni pamoja dhana Ya PPP na nafasibyake kuelekea dira ya 2050,sekta ndogobya uchumi na nafasi ya PPP katika kukuza uwekezaji na utawala bora.