Na Lucy Ngowi
“TUNATOA wito kwa wananchi wetu waweze kufika kwenye Ofisi zetu za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), kwa wakati ili waweze kutatuliwa migogoro yao ya kikazi,”.
Ofisa Mfawidhi Dar es Salaam wa ÇMA, Yohana Massawe amesema hayo alipozungumza na Mwandishi wa Mfanyakazi, mkoani Dar es Salaam.
Massawe amesema pia wananchi wanapokuwa bado wako kazini wapeleke changamoto wanazokutana nazo , kwani wengine hawana mikataba ya ajira, wengine hawalipwi mishahara inayotakiwa kisheria,
Wengine hawalipwi mishahara inayotakiwa kisheria, wengine wanapewa adhabu ambazo haziwastahili lakini wanakosa pa kupeleka changamoto zao.
“Idara ya Kazi pia ipo katika kuhakikisha kwamba viwango vya kazi vinasimamiwa kikamilifu, wafanyakazi na waajiri kila mmoja anafanya kazi yake kwa wakati wake katika viwango vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria,”amesema.
Amesema imani yake ni kwamba kila mmoja wakishirikiana mazingira ya kazi yatakuwa salama, yatakuwa ni mazingira bora.