Na Lucy Lyatuu
WAFANYAKAZI nchini wametakiwa kufahamu vihatarishi vilivyopo katika sehemu zao za kazi na kujua namna ya kukabiliana navyo Ili kuepuka madhara ya kiafya.
Wakala wa Afya na Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) umesema katika maeneo ya kazi ni muhimu mwajiri kuelimisha na kuhakikisha tahadhari zinachukuliwa.
Akizungumza katika semina ya waandishi wa Habari kutoka Chama Cha Wafanyakazi wa vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Meneja Mafunzo na Uhamasishaji Shaban Nkindi amesema hakuna kazi isiyokuwa na kihatarishi hata kama ni ndogo.
” Kwa wale waliopo ofisini muda mwingi ni muhimu kuangalia mpangolio wa Ofisi,kwamba viti wanavyokalia kama ni salama kwa Afya zao maana vingine isiwe sababu ya kuwa na matatizo ya misuli,” amesema.
Amesema kukaa muda mrefu yaani egonomia nako inaweza kuwa sababu ya Tatizo lazunguko wa damu mwilini,hi yo muhimu sana kuangalia namna ya ukaaji.
Mkindi amesema hata kama ni kazi ya kutumia nguvu,jambo muhimu ili kuwa salama kuwe na utaratibu wa kupumzika pamoja na kujinyoosha misuli.
Kwa upande wake Wakili wa OSHA, Rehema Msekwa amesema yapo masharti yanayotakiwa kuzingatia mahali pa Kazi ikiwa ni pamoja iwepo wa maji safi na salama ya kunywa,vyoo kuzingatia mahitaji na Wafanyakazi kupima afya.
Amesema wafanyakazi wakiwa salama tija inaongezeka mahala pa kazi na kwamba ni muhimu kujua Sheria ya Usalama mahali pa Kazi nba 5 ya mwaka 2003.