Na Mwandishi Wetu
RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 amewateua wafuatao kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa Ofisi Ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt Moses Kusiluka walioteuliwa ni pamoja na Dkt Dorothy Gwajima, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Balozi Dkt Bashiru Kakurwa, Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar na Dkt Rhimo Simeon Nyansaho.

