MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Waandishi wa Habari wa Afrika wapata mafunzo ya Kuandika Habari za Uhamiaji
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Waandishi wa Habari wa Afrika wapata mafunzo ya Kuandika Habari za Uhamiaji
Habari

Waandishi wa Habari wa Afrika wapata mafunzo ya Kuandika Habari za Uhamiaji

Author
By Author
Share
4 Min Read
Na Lucy Ngowi
NAIROBI – KENYA — WAANDISHI wa Habari kutoka Afrika wamekutana jijini Nairobi kwa ajili ya mafunzo kuhusu mbinu za kuandika habari za uhamiaji
Mafunzo hayo ya siku tatu yameandaliwa chini ya Mpango wa Pamoja wa Uhamiaji wa Wafanyakazi (JLMP) kwa ushirikiano na Tume ya Umoja wa Afrika, IOM, ILO na Shirikisho la Waandishi wa Habari Afrika (FAJ), yakilenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za uhamiaji kwa mtazamo wa Kiafrika na kwa kuzingatia ukweli.
Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki Edwin Righa,  amesesitiza umuhimu wa nafasi ya waandishi wa habari katika kuifanya mitazamo ya umma kuhusu uhamiaji.
“Ninyi ni watafuta ukweli, waandaaji wa ajenda na wanasimulia hadithi kwa niaba ya jamii. Nafasi yenu ni ya kipekee katika jinsi ya kuripoti uhamiaji unaeleweka na kuzungumzwa katika jamii zetu,” amesema.
Amesena Bara la Afrika linapitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi, huku vijana wengi wakihamia kutoka nchi moja hadi nyingine kutafuta ajira, heshima na maisha bora.
Amesema kuwa maelezo mengii kuhusu uhamiaji yanayotawala vyombo vya habari si ya kina na mara nyingi hujikita kwenye siasa au hofu kuliko uhalisia.
“Mara nyingi tunasimulia zaidi habari za majanga. Ingawa si vibaya, tunapaswa pia kuangazia mchango wa maendeleo unaotokana na uhamiaji,” amesena.
Righa amewataka waandishi kutumia takwimu kuandika habari zilizo bora, za haraka na za kuaminika, zitakazosaidia umma kupata taarifa sahihi zinazotegemewa.
“Mafunzo haya pia yanajengwa juu ya msingi wa Mtandao wa Waandishi wa Habari wa Uhamiaji wa Wafanyakazi wa Afrika, uliozinduliwa mwaka 2023 kwa lengo la kukuza uandishi wa habari wa kimaadili na wa ushirikiano barani Afrika.
“Ushiriki wenu unaonesha namna maono haya yanavyoimarika — kuwakutanisha waandishi na watunga sera, na kusogeza zaidi simulizi za uhamiaji kwenye maisha halisi ya wahusika,” amesema.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Kenya (KUJ), Erick Oduor ameeleza kusikitishwa kwake na hali ya habari nyingi za uhamiaji barani Afrika kuandikwa na vyombo vya habari vya kimataifa.
 “Mafunzo haya yanatufundisha namna ya kurudisha simulizi hizi mikononi mwa Waafrika na kuandika habari zinazotokana na hali halisi ya bara letu,” amesema.
Oduor ameeleza kuundwa kwa mtandao wa kikanda wenye wawakilishi saba kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki, zikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Tanzania, Sudan Kusini, Seychelles na Comoro.
Kwa lengo la kusukuma ajenda ya uandishi wa habari za uhamiaji katika kila nchi kwa kuzingatia ukweli na takwimu sahihi.
Akitoa mfano, Oduor ameeleza jinsi chama chao kilivyofanikiwa kujumuisha kipengele katika makubaliano ya kazi na shirika moja la habari la kimataifa jijini Nairobi ili kuwalinda wafanyakazi wahamiaji.
 “Tunapaswa kufikiria pia kuhusu wale wanaofanya kazi katika nchi zetu bila kuwa raia wa nchi husika. Hawa pia wanahitaji haki na ulinzi kazini,” amesena.
Oduor amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kushirikishwa tangu mwanzo wa mijadala ya sera za uhamiaji.
“Tusiwakumbuke waandishi wa habari tu kunapokuwa na janga. Vyombo vya habari ni washirika muhimu katika uundaji wa sera,” amesema.
Mafunzo hayo yataendelea kwa siku mbili zaidi, yakiwa na matarajio ya kuzalisha simulizi mpya na mtandao thabiti wa waandishi ambao wataweza kubadilisha taswira ya uhamiaji barani Afrika — kwa usahihi, kwa uhalisia na kwa athari chanya kwa jamii.

You Might Also Like

Rais Samia akunwa na Tarura

MOI Yawasogelea Dodoma, Mikoa Jirani

Ridhiwan Kikwete awasilisha taarifa mwenendo wa ulipaji mafao

Rais Samia aweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa Suluhu Sports Academy

Miaka Minne Ya Samia, TANESCO Yajivunia Kudhibiti Upotevu Wa Umeme

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article Profesa Anangisye Atoa Neno Kwa Wahitimu
Next Article Kasulu DC Yapongezwa Kwa Kupata Hati Safi
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Waziri Mkuu Majaliwa Akabidhi Tuzo kwa BoT Geita
Habari September 22, 2025
BoT Yarahisisha Uuzaji wa Dhahabu kwa Wachimbaji, Yatoa Punguzo La Mrabaha
Habari September 22, 2025
Waziri Mkuu Apongeza Huduma Kidijitali za NSSF, Maonesho Ya Madini Geita
Habari September 22, 2025
Mkuu Wa Mkoa Shinyanga Asifu Kazi Ya Bodi Bima Ya Amana
Habari September 22, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?