
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Julai 11, 2024.
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Suleiman Abubakar Mombo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa leo Alhamisi Julai 11, 2024.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mululi Majula Mahendeka na kusainiwa na Sharifa Nyanga, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Mombo amechukua nafasi ya Balozi Ali Idi Siwa ambaye amestaafu.