MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
Magazeti
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Habari Mpya
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Chagua hapa
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
  • Advertise
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Reading: Umeme Jua Kuchoche Uchumi Maeneo Ya Vijijini
Share
Notification Show More
Font ResizerAa
Font ResizerAa
MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Search
  • Home
  • Habari
  • Mfanyakazi
  • Magazeti
  • Bookmarks
Follow US
© 2022 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
MFANYAKAZI TANZANIA > Tovuti > Habari > Umeme Jua Kuchoche Uchumi Maeneo Ya Vijijini
Habari

Umeme Jua Kuchoche Uchumi Maeneo Ya Vijijini

Author
By Author
Share
3 Min Read
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI  kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imepeleka Mkoani Lindi Mradi wa Umeme Jua wenye thamani ya sh milioni 801.74 katika visiwa vyote vitano vilivyopo wilayani Kilwa .
Lengo ni kuongeza upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo ambayo yapo mbali na Gridi ya Taifa na kuhamasisha matumizi ya teknolojia safi kupitia mifumo ya umeme jua.
Akizungumza wakati akipokea taarifa ya mradi huo Katibu Tawala Mkoa wa Lindi,  Zuwena Jiri amekiri kupokea mradi huo na kutoa wito kwa wananchi mkoani humo hasa wakazi wa Visiwani kuchangamkia fursa hiyo kwani tayari Serikali imetoa ruzuku.
Habari Picha 9065
“Kila kaya itakuwa na mfumo wake wa kujitegemea, wito wangu kwa wananchi hasa wakazi wa visiwani tuchangamkie fursa iliyokuja, kama mmoja angekuwa anafunga mwenyewe mfumo wa umeme jua inawezekana ikawa gharama kubwa sana lakini Serikali imetoa ruzuku mpaka asilimia sabini na tano ,”. Amesema  Zuwena.
Pamoja na hilo Zuwena amewataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa ya Majiko Banifu ambapo serikali imetoa ruzuku ya  asilimia 85 na kufanya gharama ya Jiko moja kuuzwa kwa Shs 9000 tofauti na bei halisi ya Shs 60000.
Kwa upande wake, Meneja wa Teknolojia za Nishati kutoka REA, Michael Kyessi amesema mradi unategemea kusambaza Majiko Banifu 5,576 kwa Mkoa wa Lindi ambapo Majiko 1,115 yatagawanywa kwa kila wilaya.
“Gharama ya mradi kwa mkoa wa Lindi ni sh 346,560,000.00  ambapo Serikali itatoa ruzuku ya sh 294,576,000.00 .
Mtoa huduma ni Tango Energy Ltd ambapo jumla ya majiko banifu 5,776 yatauzwa kwa wananchi kwa bei ya ruzuku.
Gharama ya jiko moja ni sh 60,000 kabla ya ruzuku, hivyo serikali itatoa ruzuku ya asilimia 85 sawa na sh 51,000 na mwananchi atanunua jiko hilo kwa  sh 9,000.
Habari Picha 9066
Majiko haya yatasambazwa katika wilaya tano za Mkoa wa Lindi”. Amesema  Kyessi.
Kuhusu mradi  wa jua ambao utafikia kaya 1,227 ndani ya visiwa vitano mkoani humo, Kyessi amebainisha  mifumo hiyo imegawanyika katika mafungu matatu ya uwezo wa nishati ambayo ni 50Wp, 80Wp na 100Wp.
Jumla ya mifumo ya 50Wp ni 736, 80Wp ni 307 na 100Wp ni 184.
“Gharama ya ruzuku imetolewa kwa asilimia na kila atakayefungiwa mfumo wa uwezo wa Wat 50 Wp atapata ruzuku ya  asilimia 75, mfumo wa Watt 80 Wp atapata ruzuku ya asilimia  65 na mfumo wa Watt 100 Wp atapata ruzuku ya asilimia  55”. Amesema Kyessi.
Gharama za mradi kwa mkoa wa Lindi ni sh miilioni 801.74 ambapo ruzuku ni sh milioni 544.21 sawa na asilimia 68 ya gharama zote ya mradi na sh milioni 257.53 ni fedha toka kwa wanufaika.
Katika Mkoa wa Lindi mradi huo unategemea kuhudumia visiwa vitano na mtoa huduma mmoja  ambaye anategemea kuhudumia visiwa hivyo kupeleka jumla ya mifumo 1,227 ndani ya kipindi cha miaka miwili.

You Might Also Like

Wanafunzi Waliokwenda China Watakiwa Kuiwakilisha Tanzania Vizuri

TASAC yajipanga kuhudumia wafanyabiashara

Rais Samia aipongeza TPHPA, kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi, Watendaji

Tume Ya Mipango Yaelekeza Waandishi Wa Habari Kutoa Elimu Ya Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050

Serikali Yaahidi Kupatia Dawa Kilio Cha Ushuru Kwa Malori

Share This Article
Facebook Twitter Whatsapp Whatsapp Email Copy Link Print
Previous Article REA Yajivunia Mafaniko ya usambazji wa Teknolojia za Nishati Safi kwa Wananchi Vijijini
Next Article Tume Ya Mipango Yaelekeza Waandishi Wa Habari Kutoa Elimu Ya Dira Ya Taifa Ya Maendeleo 2050
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

235.3kFollowersLike
69.1kFollowersFollow
11.6kFollowersPin
56.4kFollowersFollow
136kSubscribersSubscribe
4.4kFollowersFollow
- Advertisement -
Ad imageAd image

Latest News

Majaliwa Apongeza Jeshi La Magereza Kurasimisha Ujuzi Kwa Wafungwa
Habari August 27, 2025
Mapokezi Ya Katibu Mkuu CCM  Dkt Migiro CCM, Aahidi Ushirikiano
Habari August 27, 2025
Majaliwa Aagiza Kuimarishwa kwa Mafunzo ya Ufundi Stadi Nchini
Habari August 27, 2025
VETA Yaanzisha Kozi Mpya ya Teknolojia ya Mifumo ya Viwandani
Habari August 26, 2025
//

To be acknowledged as Africa’s premier and most reliable digital media network, delivering exceptional content across all our platforms by 2025.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

MFANYAKAZI TANZANIAMFANYAKAZI TANZANIA
Follow US
© 2024 Mfanyakazi Tanzania. All Rights Reserved.
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?