DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo (ILRI), imekuwa ikisaidia maendeleo ya sekta ya kuku nchini kupitia miradi rasmi na ile isiyo rasmi katika kuwajengea uwezo na kuwawezesha wanawake na vijana.
ILRI imekuwa ikiwezesha wanawake na vijana kwenye ujasiriamali wa lishe bora unaowawezesha kuwaongezea kipato.
Ulega amesema hayo wakati wa hafla ya kutimiza miaka 50 toka kuanzishwa kwa tasisi hiyo.
Amesema kwa uwezeshaji huo wa ILRI kwa wanawake na vijana umewezesha kuwepo kwa ushirikiano katika mnyororo wa thamani wa ufugaji huo wa kuku, katika kutafuta namna ya kuimarisha ushindani wa wakulima katika eneo la lishe bora.
Amesema kampeni iliyoongozwa na ILRI na wadau wengine iliwezesha upatikanaji wa mifugo bora ya kuku inayoweza kukabiliana na magonjwa na ufugaji wenye tija.
“Asilimia 65 ya wanawake wafugaji wa kuku wa mkoani Kilimanjaro na Lindi walipata uzoefu wa namna ya kudhibiti magonjwa ya kuku, hali iliyowafanya kuongezeka kwa mifugo, kuongezeka kwa kipato na kuwa na familia bora,” amesema.
Amesema katika kusherehekea miaka hiyo 50 kwa Tanzania kama nchi imenufaika na taasisi hiyo ambapo wizara yake imekuwa ikishirikiana moja kwa moja katika shughuli zake.
“Wizara ya Mifugo na Uvuvi inafanya kazi na wadau mbalimbali washirika wa maendeleo, wafadhili, sekta ya umma na binafsi, naweza kushuhudia
kwamba ILRI imekuwa mshirika mzuri katika maeneo mengi, ikiwa ni msaada mkubwa kwa wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Utafiti Tanzania, Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).
“Mipango ambayo ILRI na washirika wake wamefanya kazi tangu uongozi wangu
kama naibu waziri wa mifugo na uvuvi hadi sasa
isiyoweza kuhesabika, lakini nitaonyesha mafanikio machache,” amesema Ulega.
Amesema mafanikio hayo ni pamoja na watumishi wa wizara yake kupata msaada wa kiufundi kutoka ILRI pamoja na msaada wa fedha kutoka kwa Bill na Melinda Gates mwaka 2016.
Pia amesema taasisi hiyo kwa kushirikiana na TALIRI wamesajili zaidi ya wanyama 69,000 kutoka makundi 33,000 mkoani Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Iringa,Njombe, Mbeya, na Songwe.
Vile vile amesema jitihada zilizofanywa na taasisi hiyo katika kuwashirikisha wanawake na vijana kumewezesha kutatua changamoto ya ajira hapa nchini.
Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu eneo la Utafiti na Ubunifu wa Mifugo ya Kimataifa kutoka ILRI, Fabian Kausche amesema wamepata heshima kubwa kuweka alama ya utendaji wao kwa miaka 50 nchini Tnzania, ambapo taasisi hiyo ilikuwepo tokea mwaka 1997.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa ILRI, Appolinaire Djikeng, Kausche amesema Tanzania ina nafasi ya pekee kutokana na ushirikiano iliyonayo na taasisi hiyo.
Amesema mkakati mpya wa taasisi hiyo ni kuboresha
maisha ya watu milioni 300 kwa kuzingatia ufugaji endelevu wa kisayansi.
“Ili kufikia hili, tutafanya kazi katika maeneo manne yaliyounganishwa ambayo yanashughulikia mifugo
maendeleo na masuala mapana kama vile afya, hali ya hewa na mazingira.
“Pia tutaelekeza juhudi zetu kimkakati zaidi ndani ya nchi kwa kuweka kipaumbele kwa minyororo maalum ya thamani iliyotambuliwa na serikali na kufanya kazi na sekta binafsi, washirika wa maendeleo na watendaji wengine wasio wa serikali kuhakikisha wana mtazamo wa pamoja na endelevu,” amesema.
Amesema ili kufungua uwekezaji katika sekta wanahitaji kusaidia serikali kuweka sera wezeshi katika mazingira ya kukuza ukuaji.
“Hili ni eneo tunalofanyia kazi,na tuko tayari kushirikiana na kuongoza.
ILRI inapitia mabadiliko mengi ya ndani ili kuhakikisha kuwa tuko kimkakati
iliyounganishwa kufanya kazi na washirika na kutoa athari ambayo sote tunataka,” amesema.