Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: MHADHIRI kutoka Idara ya Uhandisi Kilimo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Pascal Milindi amesema wamelenga kutafiti ndege nyuki zinazopunguza uchafuzi wa hewa.
Milindi amesema ndege nyuki hizo zinazotumika kwenye shughuli za kilimo katika mnyororo wa thamani wa kilimo ambao ni kumwagilizia dawa ya kukuzia miwa kwa haraka na kuongeza sukari, kwenye mashamba makubwa ya miwa kwenye viwanda vikubwa vya sukari ambavyo ni Kagera, Kilombero, Mtibwa na Manyara.
“Tulichokuwa tunafanya kwenye utafiti huu ni kutokana na mambo ya mabadiliko ya tabia nchi na hewa ukaa, sasa katika kila shghuli tunajaribu kuipunguza kadri iwezekanavyo.
“Kwenye shughuli hii ya kilimo tunajaribu kuangalia je? Matumizi ya ndege kwenye kumwagilia au kunyunyiza hizo dawa ya kukomaza miwa na tukitumia hizo drone je hii teknolojia iliyoendelea ni kweli inasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuunguza hewa ukaa, ndiyo lengo kubwa la mradi huu,” amesema