Na Lucy Ngowi
DAR ES SALAAM: “UNAWEZA kuunguliwa nyumba usiridhike, unakuja EWURA. Unaweza kujaziwa mafuta machafu, unakuja EWURA. Unaweza kujaza mafuta ambayo bei sio ile iliyotolewa na EWURA, unakuja kulalamika. Utafidiwa kutokana na kile kilichotokea, inategemeana,”.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo amesema hayo wakati wa Mafunzo ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji kwa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania ( JOWUTA).
Kaguo amesema EWURA ni taasisi inayoweza kubadilika na kufanya maamuzi ya kimahakama.

” Tunaposhughulikia malalamiko, tunabadilika na kuwa mahakama,” amesema Kaguo.
Amesema mamlaka hiyo inatatua malalamiko na kufika hadi mwisho, kwa kusimamia sheria, taratibu na kanuni.